Quantcast
Channel: Sports Lady

KOZI ZA UKOCHA ZISAIDIE KULETA MAPINDUZI KATIKA SOKA

$
0
0
Na Dina Ismail
KADIRI miaka inavyosonga  ndivyo  mwamko na chachu ya kusaka  mafanikio ya soka yanavyoongezeka.
Hilo halina ubishi kwani tumeshuhudia mengi  katika miaka ya karibuni  na mojawapo ni  kwa wachezaji wa Kitanzania kuitangaza nchi katika bara la Afrika na dunia kwa ujumla kupitia soka ya kulipwa.
Katika  harakati hizo za kusaka mafanikio, wiki iliyopita kumezalishwa makocha wapya 27 ambao walifuzu kozi ya  kati  iliyoratibiwa kwa kufuata miongozo ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) na lile la Afrika (CAF).
Kozi hiyo ambayo ilijazwa na idadi kubwa ya wachezaji  mahiri waliokuwa  wakizicheza timu kongwe za Simba na Yanga na ile ya Taifa ‘Taifa Stars’  ambapo siku ya ufungaji mgeni rasmi alikuwa  Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Malinzi alifurahishwa na idadi kubwa ya makocha waliohitimu  na na kusema kuwa itasaidia kukuza soka nchini , huku akisikitishwa  na ushiriki wa wanawake ambapo ni mmoja tu kati ya  27 aliyejitokeza na hivyo kutoa rai kwa wanawake kujitokeza kwenye kozi za namna hiyo.
Kujitokeza kwa nyota hao wa zamani kushiriki kozi hiyo ni jambo la  kupongezwa kwani  inaonesha  ni jinsi gani wana uchungu na maendeleo ya nchi yao hivyo wameona kufanya hivyo kutasaidia kwa namna moja ama nyingine.
Ikumbukwe, wengi wa washiriki wa kozi hiyo walipata kutoa mchango mkubwa katika soka Tanzania enzi za uchezaji wao hivyo naamini kupitia mafunzo hayo pamoja na uzoefu walionao wa kisoka kutasaidia kupatikana kwa wachezaji bora zaidi chini ya mikono yao.
Hata mwanamama pekee aliyeshiriki kozi hiyo, Doris Malyaga ambaye ni mwandishi wa habari za michezo nchini, mbali na ukufunzi huo pia ataitumia vema kalamu yake katika kuhamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi katika kozi kama hizo.
Hii in maana kwamba, kama kutakuwa na makocha wengi wanawake wenye viwango na  utaalamu wa hali ya juu ni wazi kwamba itapunguza idadi ya makocha wa kiume katika timu za wanawake.
Hivyo basi  mafunzo waliyoyapata yasiishie kuwavimbisha vichwa, vyeti walivyoviopata visiwe mapambo katika kuta za nyumba zao bali wayatumie kuwafunza  wachezaji  wenzao na hasa timu za vijana ambazo ni muhimu sana katika mustakabali wa matunda ya baadae.
Kama hiyo haitoshi, makocha hao wapya wasibwetye na kozi hiyo  hivyo wanawajibu wa kujingeza zaidi ili kuweza kufikia katika madaraja ya juu  ili siku zijazo Tanzania itanue wigo wa kuwa na makocha wanaofundisha nje ya Tanzania.
Baada ya hatua hiyo naamini kila mshiriki wa kozi hiyo hatobweteka na hatua hiyo hivyo atakuwa na jukumu la kujiongeza zaidi ili kupanda daraja.
Kozi hiyo iliendeshwa na   mkufunzi anayetambuliwa na  CAF Wilfred Kidao,  akisaidiwa na kipa mkongwe wa zamani  Manyika Peter aliyefundisha  mtaala kwa makocha wa makipa,  Dk. Nassoro Ally Matunzya aliyefundisha  kuhusu tiba za wanamichezo/wanasoka  pamoja na mMkufunzi wa muda mrefu wa soka, Hemed Mteza.
Mbali na Malyaga , washiriki wengine walohudhuria  kozi hiyo ya siku 14 ni pamoja na  Boniface Pawasa, Fred Mbuna, Innocent Haule, Herry Morris, Ivo Mapunda, Nizar Khalfan na Mussa Hassan Mgosi.

Wengine ni Omar Kapilima, Amosi Mgisa, Uhuru Mwambungu, Yussuf Macho, George Minja, Haruna Adolf, Selemani Omari, Ally Ruvu, Masoud Selemani, Haji Mustapha, Mhasham Khatib, Issa Ndunje, Salum Kapilima, Said Salum, Julio Elieza, Hassan Mwakami, Rajab Mponda, Ally Mbonde na Evod Mchemba.

LIPULI FC IRUDI NA MOTO WA ZAMANI LIGI KUU

$
0
0
Na  Dina Ismail

BAADA ya kutoshiriki Ligi Kuu soka Tanzania Bara kwa takribani miaka 17, hatimaye timu ya Lipuli ya Iringa imekata tiketi ya kucheza ligi hiyo msimu wa 2017/18.

Lipuli  iliyokuwa tishio katika miaka ya nyuma kwenye soka, imekata tiketi hiyo baada ya kufikisha pointi 29 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote katika kundi A huku ikibakiwa na michezo miwili.

Chini ya kocha wake mkuu, Richard Amatre ambaye ni raia wa Uganda, timu hiyo ilianza kuonesha dalili za kupanda daraja tangu kuanza kwa ligi hiyo ambapo iliweza kufanya vema katika michezo yake.

Amatre ambaye alipata kuwa kocha msaidizi wa Simba, amekuwa akijigamba kwa timu yake kufanya vema na kweli ndicho kilichotokea na hivyo kuifanya timu yake kupanda daraja.

Kocha Amatre ambaye amedumu na timu hiyo kwa miaka mitatu pamoja na kuwapongeza wachezaji wake kwa hatua hiyo anasema haikuwa rahisi kwao kuibuka vinara katika kundi lao.

Lipuli ambayo miaka ya nyuma ilipokuwa ikishiriki Ligi Kuu Bara ilikuwa ni moja ya timu tishio sana, haijapanda kirahisi kwani kabla ya mwaka huu ilikuwa ikiishia nafasi ya pili na tatu.

Ni moja ya timu iliyokuwa na heshima kubwa Tanzania; mkoa wa Iringa una matajiri wengi ambao kama wakiamua wanaweza kuihudumia timu hiyo na kuepuka vishawishi hivyo vya timu kubwa na kutoa upinzani mkubwa kwa Yanga na Simba zinapokwenda kwenye uwanja wa Samora pale Iringa.


Enzi hizo, hakuna mshabiki wa soka aliyekosa kuifahamu Lipuli kwani haikuwa timu ya kawaida kwa kutandaza kabumbu safi kupitia kwa nyota wake waliokuwa na uwezo wa hali ya juu.

Kama hiyo haitoshi, Lipuli ilikuwa ni roho ya Wana Iringa kwani ni timu pekee iliyokuwa ikiuwakilisha vema mkoa huo, hivyo ni wazi kwamba wakali hao wa zamani wataendeleza makali yao ya zamani.

Kwamba, lengo lao la kufanya mapinduzi ya soka kwa mkoa wa Iringa liendane sambamba na kufanya vema katika Ligi Kuu Bara kwani kinyume na hapo itakuwa ni kazi bure.

Kupanda kwa Lipuli ni nafasi pekee kwa wakazi wa mkoa wa iringa pamoja na wadau wa soka kuhakikisha wanaiunga mkoni na kuipa sapoti timu hiyo ili iweze kudumu na siyo kupanda na kushuka.

Matajiri wa Iringa wanatakiwa kujitolea kuisaidia timu hiyo iweze kujimudu na kuondokana na ukata ambao unaweza kuitia timu hiyo majaribuni kwa wachezaji kupokea rusha na kupeleke timu hiyo kupoteza mwelekeo kwenye ligi ya msimu ujao.

Lakini kitu kingine ambacho ni chamuhimu zaidi kwa timu hiyo ni kuepuka kufungamana na upande mmoja katika ya timu mbili kubwa za Simba na Yanga na kujenga timu isiyofungamana na upande wowote kati ya hizo mbili.


Timu nyingi kwenye ligi ya Vodacom zimekuwa zikiathirika kwa jambo hilo la kufungamana na upande mmoja kati ya timu hizo mbili, na hali huwa mbaya na wakati mwingine kushuka daraja pindi timu kubwa inapohitaji pointi tatu ili kutwaa ubingwa au nafasi fulani kwenye msimamo .

YANGA TULIENI VINGINEVYO MTAZIDI KUPOTEA

$
0
0

Na Dina Ismail

KUMEKUWA na sintofahamu katika klabu ya soka ya Yanga kufuatia taarifa za kuwepo kwa hali ya ukata unayoikabili.

Hali hiyo inafuatia mwenyekiti na mdhamini wa timu hiyo, Yussuf Manji kuwa katika misukosuko baada ya akaunti zake kufungwa na serikali.

Kwamba, Manji baada ya kukumbwa na misukosuko hiyo klabu imekuwa katika hali mbaya ya kifedha  ambapo Katibu mkuu wa Yanga   Charles Boniface Mkwassa akithibitisha hali hiyo.

Kama hiyo haitoshi, ukata huo umepelekea Yanga kusitisha ajira ya Mkurugenzi wake wa ufundi, Hans Van Pluijim.

Pia kuna taarifa ya baadhi ya wachezaji kwamba wapo mbioni kuikimbia klabu hiyo kutokana na hali mbaya ya kiuchumi iliyonayo.

Hizi dalili mbaya kwa klabu ya Yanga na isipochukuliwa tahadhari ni wazi kwamba itapoteza hata matumaini yake ya kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara na hata michezo yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga ni mali ya wanachama hivyo basi ni wajibu kwa kila mwanachama  mwenye mapenzi ya kweli kujitoa kwa hali na mali kuhakikisha wanaiokoa klabu yao ili iweze kurudi katika mstari.

Kuendelea kuacha jukumu la kuiendesha pekee kwa uongozi itakuwa ni kuwatwika mzigo ambao hawawezi kuubeba.

Pia ni wakati kwa viongozi kuamka katika usingizi wa muda mrefu iliokuwa imelala kwa kutegemea mtu mmoja katika kuindesha kwenye masuala ya kiuchumi.

Yaangi, viongozi wapigane kufa kupona ili kuhakikisha wanapatikana wafadhili ama wadhamini ambao watamwaga fedha kwa ajili ya kuindeshe klabu hiyo.

Soka la sasa lipo kibiashara zaidi, hivyo bila ya kuwa na fedha itakuwa gumu kwa klabu kubwa kama Yanga kuishi kwa kutegemea mapato ya mlangoni tu.

Kwamba , tahadhari zisipochukuliwa ni mengi tutayasikia na kuyaona kwani Yanga imesheheni wachezaji wa kigeni ambao wanahitaji kulipwa mishahara na stahiki zao nyingine, hata wale wazawa pia wanahitaji kulipwa hivyo bila pesa kuna kitakachochezwa hapo?

Tukirejea historia ya soka la bongo inaonesha kwamba, dalili za namna hii na hasa kwa vilabu vikubwa kama Yanga ni mbaya na zisipofanyiwa kazi zitawagharimu sana na itawachukua muda mpaka kukaa katika mstari ulionyooka.

Yanga ambayo pia inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika inahitaji kujiaandaa vema ili kuweza kushinda michezo yake na kusonga mbele na maandalizi hayawezi kuwa bora bila ya kuwepo kwa fedha.

Ni kipindi ambacho ‘vivuruge’ watakitumia kwa lengo la kuhakikisha Yanga inaparaganyika hivyo kushindwa kutimiza harakati zake za kutetea ubingwa.

Katika kipindi hiki cha mpito ni vema kukawepo na amani na mshikamano ili mwisho wa siku lolote litakalotokea libaki kuwa limetokana na umoja huo.

Bila mshikamano ni wazi kwamba mtavuruga hadi akili za wachezaji wenu na hivyo kupelekea kupoteza mwelekeo kabisa katika kutimiza wajibu wao .

Shime kwa wanaYanga kuchukua tahadhari mapema kabla ya hatari kubwa inayioweza kuja kutokea katika siku zijazo.

TUCHAGUE VIONGOZI BORA ILI TUPIGE HATUA MICHEZONI

$
0
0
Na Dina Ismail

KWA miaka mingi Tanzania imekuwa  ikifanya vibaya katika michezo mbalimbali ya kimataifa ambayo inashiriki.

Licha ya kujaliwa kuwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu lakini bado hali imekuwa si ya kuridhisha kabisa.

Hata hivyo sababu  hasa ya kutokufanya vema  na kujikuta kuwa wasindikizaji tu katika mashindanio tunayojaliwa kushiriki bado haijajulikna.

Kwani kama ni maandalizi hufanyika ya kutosha, kama ni walimu wapo wazuri sana iwe wazawa ama wale wa kigeni ambao naamini hawana tofauti na wan chi nyingine.

Ukiangalia kwa haraka haraka, kitu kikubwa kinachotukwamisha ni viongozi tulionao katika ngazi mbalimbali.

Ndio! Viongozi ndio kila kitu katika mafanikio ya kitu hivyo basi tunaweza kusema wao ndio wanachingia tufanye vibaya au vizuri katika michezo.

Sifa ya kiongozi bora ni kuhakikisha anasimamia vilivyo anachokiongoza ili mwisho wa siku kiwe kitu bora na chenye manufaa kwa Taifa.

Na viongozi wengi wa vyama vya michezo hawana sifa za viongozi kwani uwepo wao umetokana na shinikizo kutokana na sababu fulani, ushabiki na mengineyo.

Kwamba wengi wa viongozi katika michezo hawana wapo kwa manufaa yao binafsi na si katika kuendeleza michezo.

Tumesshuhudia katika kampeni kabla ya chaguzi mbalimbali, viongozi wengi wakitoa ahadi nzuri sana na za kupendeza na kuwavutia wapiga kura lakini pindi wanapochaguliwa hushindwa kutekeleza.

Hivyo basi, kushindwa kwao kutekeleza ahadi walizoweka pindi wanaomba kura ndiyo inakuja pelekeakubaki wasindikizaji katika michuano ya kimataifa.

Kiongozi anaonekana kipindi cha kuomba kura tu na baada ya hapo humuoni ofisini wala kwenye viwanja vya michezo kwa ajili ya kutoa sapoti ama neno lolote la faraja kwa wanamichezo wa eneo lake.

Kiongozi hajui hata wanamichezo ama michezo iliyopo katika eneo lake, yeye huishia kuja kutoa pongezi kwa washindi au kuzindua mashindano tu.

Kuna maeneo yamebarikiwa kuwa na hali nzuri ya hewa kwa ajili ya wanamichezo kufanya maandalizi yao lakini kutokana na kuwa na viongozi wasiokuwa na kiu ya mafanikio wanashindwa kuzitumia vema rasilimali hizo.

Ifikie mahala wapiga kura wajiongeze kwa kuchagua viongozi ambao wana lengo na dhamira ya dhati kabisa ya kuinua na kuendeleza michezo na si kuchagua viongozi ‘wauza sura tu’.

Kwamba, kiongozi anamwaga sera za kuvutia na anachaguliwa kwa kura nyingi, lakini anamaliza muda wake bila kuleta mafanikio yoyote halafu anakuja kuomba tena nafasi ya kuongoza, huyo hafai kabisa kurudi.

Kama kweli tunataka mafanikio katika michezo ni vema wapiga kura kuchagua viongozi wanaoona wana dhamira ya dhati na uchungu na maendeleo ya soka.


Pia kwa wale viongozi maslahi ifikie mahala waone aibu kwa kujiweka kando na kuwaachia wenye moyo wa dhati kuongoza.

SIMBA, YANGA ACHENI MAMBO YA KIZAMANI

$
0
0
Na Dina Ismail

IMEKUWA ni  mazoea kwa timu vigogo nchini, Simba na Yanga kutoa ‘kafara’ watu baada ya michezo baina yao.

Tabia hiyo imekuwa ikiota mizizi kadiri miaka inavyosonga ambapo kadhia hiyo huwakumba viongozi,wachezaji na wakati mwingine makocha.

‘Kafara’ hilo hufanywa zaidi kwa timu ambayo itakuwa imefungwa.

Hivi karibuni, Yanga iliachana na Mkurugenzi wake wa Ufundi, Mholanzi Hans Van Der Pluijim kwa madai ya kwamba inakabiliwa na ukata.

Pluijim alipata kuwa kocha mkuu wa Yanga kwa nyakati tofauti kabla ya mwaka jana mkataba wake kusitishwa tena baada  ya kutoka sare  ya bao 1-1 na Simba katika ambayo Yanga ilistahili kuibuka na ushindi.

Katika mechi hiyo ya msimu uliopita Yanga ilianza kufunga kupitia Hamis Tambwe, huku Simba ambayo ilicheza ikiwa pungufu baada ya nahodha wake Jonas Mkude kutolewa kwa kadi nyekundu, ilisawazisha katika dakika za majeruhi kupitia kwa Siza Kichuya.

Hivyo matokeo hayo yali[pekea uongozi wa Yanga kumleta  kocha Mzambia George Lwandamina na hivyo Pluijim kuamua kusitisha mkataba wake.

Hata hivyo zilifanyika busara toka kwa wadau wa Yanga na hatimaye waliweza kumshawishi na kubaki kama Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo.

Kutemwa kwa Pluijim kunakuja siku chache baada ya Yanga kupoteza mchezo wake dhidi ya mahasimu wao Simba baada ya kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Hivyo basi, Yanga imeamua kumtoa Pluijim kafara kutokana na kipigo hicho na suala la ukata limewekwa kama ni sababu tu.

Inawezekana kweli Yanga wanakabiliwa na ukata kiasi cha kushindwa kumlipa Mholanzi huyo, lakini kwa kumtimua kipindi  baada ya kufungwa na Simba ni lazima tuamini kuwa ametolewa ‘kafara’.

Tukirejea historia za timu hizo zinapokutana lazima timu itakayofungwa kutatokea timuatimua au kusimamishwa kwa wachezaji au viongozi wa benchi la ufundi kwa madai kuwa walihujumu.

Kabla ya michezo baina yao huwa kuna tambo nyingi sana toka kwa kila pande huku kila mmoja akijinasibu ya kwamba yeye ni bora zaidi ya mwenzake.Sasa inakuwaje timu ikifungwa inadai kulikuwepo na hujuma?

Mpira una matokeo matatu;kufunga, kufungwa na kutoka sare, sasa Simba na Yanga kwa nini huwaga hamuamini matokeo ya kufungwa ambapo timu itayofungwa eti wamehujumu.

Hayo ni mambo ya kizamani na yaliyopitwa na wakati,haiwezekani kila mkutanapo timu ikifungwa mnahujumiwa.

Ikumbukwe kuwa mechi baina ya mahasimu kuna mambo mengi yanatokea, kuna kuzidiwa na mpira, kuna wachezaji kutokuwa vema kisaikolojia na mengineyo mengi hivyo ni wajibu kila upande kupokea matokeo yoyote itakayoyaopa.

Labda itokee suala la maamuzi ya uwanjani kuwa ya upendeleo wa wazi kwa timu moja na kupelekea ushindi hapo ndio mnaweza kuhoji lakini si kutimua ama kusimamisha wachezaji au viongozi pindi  timu inapiopoteza.

Ifikie mahala mbadilike na kuachana na mawazo ‘mgando’ yenu hayo kwani pia yanachangia kuwapoteza katika mechi zenu mingine.

Baada ya mechi kila timu ikubali matokeo na mambo mengine yaendelea na sio kukaa mnafanya uchunguzi nani chanzo cha kufungwa.


Yanga kumbukeni mna mchezo wa Ligi ya mabingwa hivi karibuni na pia mnaharakati za kutetea ubingwa, mkiendekeza kutafuta wa kumtoa ‘kafara’ mtajikuta mnapotea kila mahali.

'KIKI NI UFINYU WA MAWAZO'

$
0
0
Na Dina Ismail

HIVI karibuni  kumeibuka tabia inayokera na  kuchefua inayofanywa  na  baadhi ya  wasanii wa filamu au wale wa bongo fleva , ikijulikana kama Kiki.

Kitendo hicho kimekuwa kikitumika zaidi pindi wanapokaribia kutoa nyimbo zao au filamu zao.

Si  jambo baya kwao  kutafuta ‘attention’ katika kuelekea kuachia kazi zao mpya lakini njia wanazozitumia ni  mbaya na sio za kuridhisha.

Msanii kama kioo cha jamii hana budi kufanya ama kuonesha vitu vizuri ili awe mfano bora kwa wanaomzunguka lakini si kwa baadhi ya bongo.

Utakuta msanii anamtukana mwenzake matusi  mazito katika mitandao ya kijamii ama vyombo vya habari au msanii anaweza mzulia mwenzake jambo lolote la fedheha kiasi cha kuleta picha mbaya katika jamii lakini mwisho wa siku inakuja bainika kwamba ilikuwa ni Kiki ya kutoa kazi yake mpya.

Tumeshuhudia wasanii wakifanya mambo ya aibu sana katika mitandao ya kijamii kinyume na mila na desturi za Kitanzania na yote hayo wanafanya katika kutafuta umaarufu.

Kweli sasa hivi sanaa imekuwa ngumu kutokana na hali ya kiuchumi na pia uwepo wasanii wenye vipaji wanaochipukia kila kukicha kiasi cha kufanya sanaa iwe ngumu.

Na kwa hali hiyo ndipo wasanii hutafuta njia mbadala za kujiweka matawi ya juu kwa niia zisizo sahihi ambazo mwisho wa siku inakuwa ni kama dhalili kwao.

Kinachoonekana hapa ni ufinyu wa fikra na mawazo  pia katika kutayarisha hadi kupakua kazi zao kwani kama msanii yuko vizuri katika fikra hizo hawezi ‘kutafuta kiki’ ili atoe albamu ama filamu.

Usanii ni kipaji sasa kama kuna walioingia katika sanaa kwa lengo la kusaka umaarufu au kuuza sura ndio hao mwisho wa siku wanafanya mambo ya ajabu ajabu.

Mbona kuna wasanii wengi wanafanya sanaa kwa muda mrefu na majina yao yapo juu na hata siku moja huwakuti ama kuwaona wakitafuta ‘kiki’ za kijinga wao wanapata umaarufu kulingana na kazi zao.

Wasanii kama Mwana Fa, Fid Q, Lady Jaydee, Riyama Ali, Joh Makini, King Majuto ni baadhi ya wale wanaojielewa kwani hata siku moja huwezi sikia wanatafuta ‘kiki’ wakianza kutoa kazi zao.

Sana utaona matangazo ya ujio wao mpya, na pindi kazi ikitoka kama ni nzuri itachukua nafasi yake kupitia mashabiki na mwisho wa siku heshima yao inabaki kuwa juu.

Pia kuna wasanii walioibuka miaka ya hivi karibuni kama Darassa, huyu ni mmoja wao ambaye ubora wa kazi zake umeweza kumuweka katika matawi ya juu ya muziki wa kizazi kipya.

Kuna njia nyingi za maana na zenye heshima wanazoweza kupitia katika ‘kuprome’ kazi zao kama ilivyo kwa wasanii wan chi zilizoendelea badala ya hizi za aibu wanazozidumia baadhi yao hivi sasa.

Nadhani ifikie mahala wasanii wanaoishi kwa ‘kiki’ kujipanga upya  kuumiza vichwa kwa kutayarisha kazi  nzuri na zinazoendana na maadili ya kitanzania, kinyume na hapo naliona anguko la baadhi yao.


Mungu Ibariki Tanzania.

TIMU ZA LIGI KUU ZIWEKEZE ZAIDI KATIKA TIMU ZA VIJANA

$
0
0
Na Dina Ismail

SHIRIKISHO la  soka Tanzania (TFF) miaka kadhaa iliyopita liliweka kanuni ya kila timu inayoshiriki ligi Kuu soka Tanzania Bara kuwa na timu za Vijana, yaani ile ya miaka chini  ya 17 na 20.

TFF ilifanya hivyo kwa minajiri ya kuinua na kuendeleza soka la Tanzania, pia kusaidia kupatikana kwa hazina ya wachezaji kwa ajili ya baadaye.

Kama hiyo haitoshi, ilianzisha ligi maalum ya timu hizo za vijana ambayo imekuwa ikifanyika kipindi ambacho mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara unakuwa umesimama.

Kwa kiasi kikubwa michuano hiyo imekuwa ikileta na msisimko mkubwa kutokana na wachezaji wa timu husika kuonesha vipaji vya hali ya juu.

Pia kupitia michuano hiyo, kumetoa nafasi kwa viongozi wa timu zao kuona wachezaji ambao wanafaa kupandishwa hadi timu za wakubwa.

Lakini, ukiangalia ama kufuatilia kwa umakini utabaini kwamba baadhi ya timu hizo za vijana ‘zipo zipo’  kwani hata lengo la kuinua na kuendeleza vipaji halitiliwi maana.

Kwamba, timu za vijana zipo lakini kipindi cha usajili viongozi wanahaha kusaka wachezaji toka Simba, Yanga, Azam, Kagera Sugar na kadhalika badala ya kupandisha wachezaji wa timu zao za vijana.

Ni sawa kwao kusaka wachezaji wenye uzoefu, lakini angalau wangekuwa wanachukua hata wachezaji watano kutoka katika kikosi cha cha vijana na kasha nafasi zingine ndio kusaka magwiji na wale wa kigeni.

Kwani bila ya kuwapandisha katika kikosi cha wakubwa itakuwa ni sawa na kuuwa vipaji vyako na kuzidi kudumaza soka la Tanzania.

Kama hiyo haitoshi, kupandisha daraja wachezaji wa timu hizo za vijana kutasaidia kubana matumizi kwa kiasi fulani kwani tumeshuhudia mamilioni ya pesa yakitumika kusajili wachezaji wazoefu na wale ‘mapro’.

Swali la kujiuliza, kuna faida gani ya kuwa na timu za vijana kama hawawezi kupandishwa madaraja, mwisho wa siku inakuwa mchawi wa soka ni timu zenyewe kwani zinashindwa kuvuna matunda yake na kwenda kusaka ya nje.

Angalau tunaona baadhi ya wachezaji waliopandishwa kutoka timu za vijana wakichanua katika timu zao kwa misimu kadhaa lakini baada ya muda wanapotea katika medani ya soka.

Baadhi ya wachezaji kama Frank Domayo , Haruna Chanongo, Ramadhan Singano, Jonas Mkude, Hassan Isihaka, Peter Manyika na wengineo ni baadhi ya matunda ya timu za vijana katika Ligi Kuu Bara.

Kama hiyo haitoshi, majina ya wachezaji hao yalikuwa chaguo la mara kwa mara katika vikosi vya timu ya Taifa kwa nyakati tofauti.

Sijui tatizo ni nini, kwani kwa sasa moto wa nyota hao chipukizi umezimika ghafla na wengi wameachwa katika timu zilizowapandisha, huku wengine wakiishia kukosa namba katika kikosi cha kwanza.

Na kwa hali ilivyo itawawia vigumu sana kurejesha hadhi yao kama ilivyokuwa mwanzo na hiyo inatokana na mfumo wa soka la Tanzania ulivyo.

Tulitaraji viwango vyao vingedumu kwa muda mrefu kama ilivyokuwa enzi za kina Sekilojo Chambua, Madaraka Suleiman, Mohammed Manyika, George Masatu, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ na wengineo, lakini imekuwa tofauti na sasa hivi tunaweza kusema  ‘wapo wapo’.

Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta ni mfano wa kuigwa kwa wachezaji ‘chapuo’ la timu za vijana, kwani hawa wana vipaji pia kama walivyo wenzao lakini wasimamizi wao walisoma alama za nyakati, na leo hii ni ‘habari nyingine’.

Nadhani ni wakati muafaka kwa vilabu vya ligi kuu kuiga wa nchi zilizopiga hatua katika medani ya soka ambazo kuwapa nafasi zaidi wachezaji vijana ambao wakisimamiwa vema wataleta manufaa katika siku za usoni.

Tunaona wachezaji wengi nyota wa Ulaya wameibuka wakiwa wadogo na wamejitahidi kwa kiasi kikubwa ‘kumantain’ viwango vyao kwa muda mrefu na hatimaye ili tuweze kuwa na mafanikio katika soka.

Lakini kwa Tanzania bado hatuwatilii maanani wachezaji chipukizi,na tumekuwa tukikumbatia wachezaji wakongwe tu ambao baadhi yao hawana hata viwango vikubwa kama ilivyo kwa vijana lakini tunaona wakipewa nafasi.

Kwani hata hao waliobahatika kuwemo wameshindwa kulelewa ipasavyo matokeo yake wamejikuta wakiishia katika pasi na kufika safari yao.

Kwa hali hiyo nashindwa kuelewa faida ya kuanzishwa kwa timu B maana uwepo wake ni kama kutimiza wajibu tu!



WASANII, WANAMICHEZO WATHAMINIWE

$
0
0

Na Dina Ismail

TANZANIA  ni moja ya  nchi zinazoaminika na kusifika  kuwa  na  watu wenye amani, upendo na ushirikiano.

Kweli!  tunasifika kwa hilo toka kwa watu wa nje, lakini kwa kiasi kikubwa hali hiyo haipo baina yetu katika baadhi ya makundi ya kijamii.

Tukiangalia  katika  sekta  ya sanaa na  michezo  suala la kutowathamini watu hao lipo na linaendelea kushika kasi kila kukicha.

Hapa kwetu,msanii au mchezaji anakuwa  anathaminiwa au kupendwa pindi  anapokuwa  mzima wa afya  na mwenye nguvu zake.

Tofauti na nchi za wenzetu ambazo hata kama zina machafuko lakini wasanii na wanamichezo wanathaminiwa katika hali zote mradi tu amepata kutoa mchango wa kisanaa na michezo katika nchi yake.

 Kwamba, kwa Tanzania thamani ya wasanii na wachezaji  inaonekana pindi wanakuwa katika uzima na afya njema lakini  wakipatwa na ugonjwa au umauti hakuna anayejali.

Tumeshuhudia mara kwa mara taarifa za wasanii na wanamichezo kuomba msaada wa matibabu wanapopata maradhi lakini mapokeo ya maombi yao huwa si ya kuridhisha.

Matokeo yake jukumu la kuuguza hubaki kwa wanafamilia na kwa bahati mbaya kuna wanaofikwa na umauti au kilema kutokana na maradhi yao na hakuna anayejali.

Kama hiyo haitoshi, kuna baadhi ya wachezaji wamejikuta wakikatiza ndoto zao baada ya kuumiwa wakizitumikia timu zao na bila huruma wanatelekezwa bila msaada wowote  kubaki wakijiuguza wenyewe.

Hili linasikitisha sana, kwani pamoja na mchezaji kuumia akiwa chini ya himaya yako bado unamuacha akahangaike kujitibia mwenyewe sasa hapo thamani yake iko wapi.

Kwamba, utaona ufahari kujitokeza katika msiba wake na kutangaza kuwasilisha kiasi kadhaa cha ubani,hilo hata mungu hapendi kwani kama mlikuwa mnamthamini mngemuhudumia kuanzia mwanzo mpaka pale ahadi yake itakapofika.

Hebu tuachane na roho za kikatili kwa watu wetu hawa kwani kwa namna moja ama nyingine wanasaidia kuitangaza nchi, wanasaidia kukupa wewe kula, wanasaidia kukupa  wewe heshima, wanatoa burudani, wanaelimisha na mengineyo mengi.

Pamoja na yote mazuri na michango yao katika jamii lakini hatuwathamini kama inavyostahili kulingana na waliyoyafanya wakati wa uzima au uhai wao.

Kama hiyo haitoshi, kuna wengine wanakumbwa na umauti na hata timu, taasisi au kundi alilokuwa akilifanyia kazi linashindwa hata kuhudhuria katika msiba wake.

Basi umeshindwa kuhudhuria msiba, mfano mchezaji huyo alipata kuwa tegemeo katika timu yako na kucheza kwa mafanikio leo anazikwa na timu yako inacheza lakini unashindwa hata kusimama kwa dakika moja tu kumuombea.

Watanzania tubadilike kwa kuthamini na kujali wenzetu!




SIMBA NA YANGA ZINAONGOZA KWA KUUA VIPAJI VYA WACHEZAJI NCHINI

$
0
0
Na Dina Ismail

LICHA ya ukongwe  na umaarufu ilizonazo , vilabu vya Simba na Yanga vinaongoza kwa kuua vipaji vya wachezaji hapa nchini.

Ndiyo! Simba na Yanga ambazo ni mahasimu wa jadi nchini zinaongoza kwa kuua vipaji na kama wachezaji wasiposhtuka mapema tutapoteza vipaji vingi.

Timu hizo zenye umri wa miaka 80 tangu kuanzishwa kwake, zamani zilikuwa na historia nzuri ya kulea wachezaji wenye vipaji kwa muda mrefu tofauti na sasa.

Sijui ni utandawazi,  kukua kwa soka au  ulimbukeni  ndio kunakopelekea hali hiyo kwani hali hiyo imekuwa ikishika kasi kila uchwao.

Tanzania imejaaliwa kuna na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu lakini wengi wao wanajikuta wakipotea baada ya kujiunga Simba au Yanga.

Ukiangali kwa haraka haraka , kuna wale ambao walipitia katika vituo vya kukuza na kuendeleza soka za vijana au walipandishwa toka katika timu za vijana na kusajiliwa kuzicheza klabu hizo.

CHANZO:

Vilabu hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa fedha, hufanya kila jitihada za kusajili wachezaji wazuri kwa lengo la kuimarisha vikosi vyao katika michuano mbalimbali.

Kamati za usajili za kila klabu zitaingia msituni kusaka wachezaji wazuri ambao wanaona watafaa kuzichezea.

Hapo  sasa kuna makundi mawili,  kuna walio kwa ajili ya kuzichezea tu klabu hiyo ili kujipatia umaaarufu na pesa na kuna kundi la ambao  wapo wenye malengo ya kufika mbali kupitia vilabu hivyo.

Katika hilo; mchezaji huyo atasota mchangani , wilayani na hata mkoa akijifua na hatimaye kuonwa na moja ya timu za Ligi Kuu na kusajiliwa.

Ataichezea  kwa nguvu zake zote timu yake hiyo iwe ya daraja la kwanza au ligi kuu.Lakini akili yake ni kusajiliwa Simba au Yanga!

Baada ya kusajiliwa na moja ya vigogo hao huko ataenda kukutana na changamoto nyingi ambazo bila umakini atajikuta ndio basi tena.

Kuna ambaye atafanikiwa kuingia kikosi cha kwanza, kuna atakayebaki  kwa ajili ya mazoezi tu, sasa bila kuchekecha akili ndio itakuwa mwisho wake.

Kundi la Pili linaundwa na wachezaji ambao wanajielewa.Haijulikani kapitia njia ipi mpaka kusajiliwa Simba au Yanga.

Yeye akili yake ni kufika mbali katika medani ya soka, huyu hata akikumbana na changamoto kwenye vilabu hivyo atakabiliano navyo na mwish wa siku atafanikiwa tu.

Hii ndio aina ya wachezaji wanaofika mbali kwani baada ya kuingia katika utawala wa Simba na Yanga.

Na tumeshudia kuwepo kwa baadhi ya wachezaji ambao  hucheza kwa nguvu zote hasa pale timu yake inakapokutana na Simba au Yanga,atafanya kila awezalo ili aweze kuvutia na kesho atafutwe.

Hapo inaonesha lengo la wachezaji wengi ni kuzichezea Simba au Yanga na sio kuwa mchezaji mwenye lengo la kufika mbali.

Tabu inakuja atakaposajiliwa changamoto atakazokutana nazo Simba au Yanga ndizo zitakazomfanya abaki kikosi cha kwanza au asugugue benchi na kujibidiisha zaidi ili siku moja afanikiwe kusonga mbele.

Sio rahisi  kupata namba katika kikosi cha kwanza kama alivyofikiria kabla.Hiyo inatokana na kila idara kusheheni wachezaji wazuri na wenye uwezo wa hali ya juu.

Hapo inakuwa kama wanacheza bahati nasibu kwani kila mwenye bahati ndiye atakayekuwa chagua la kocha na hivyo kupata  namba katika kikosi cha kwanza.

Kwa mchezaji mwenye malengo kama hatobahatika kuingia kikosi cha kwanza, atashtuka mapema na kujiongeza zaidi ili aweze kutimiza lengo lililompeleka hapo.

Lakini kuna watakaobweteka kwa kuendelea kusugua benchi, mradi mwisho wa mwezi ATM inasoma yeye hajali.Mwisho wa siku unakumbwa na fagio mwisho wa msimu.

Wachezaji wengi wa Tanzania wanapotea baada ya kuingia Simba au Yanga  kwani huko watakutana na kila aina ya tabia ambazo zinasababishwa na umaarufu walionao, uwezo na uzoefu.Hivyo baadhi hujisahau!

Suluhisho


Mchezaji anatakiwa kutumia akili ya  ziada ili kuweza kufika mbali kinyume na hapo itabaki katika historia tu.

KUTOFANYIKA TAIFA CUP KUMEUA HAMASA YA SOKA MIKOANI

$
0
0
Na Dina Ismail
KWA karibu  takribani miaka minne sasa, michuno ya soka ya kombe la Taifa  maarufu kama ‘ Taifa Cup’ imeshindwa  kufanyika.
Michuano hiyo ambayo ambayo ilianzishwa waka 1964 ikijulikana kama  Sunlight Cup ilikuwa na lengo la  la kuvumbua na kukuza vipaji vya  vilivyojificha katika mikoa hiyo.
Pia michuano hiyo ililenga kuamsha na kuhamashisha michezo na hasa mpira wa miguu katika mikoa hiyo kwa lengo la kupata wachezaji ambao baadae wataunda kikosi cha timu ya Taifa ya Bara ambacho kitaiwakilisha nchi katika michuano ya Chalenji.
Kupitia michuano hiyo tumepata kushuhudia kuibuka kwa wachezaji mbalimbali ambao leo hii wameweza kuandika historia katika ramani ya soka hapa nchini.
Kama hiyo haitoshi mivhuano hiyo imeweza kuleta hamasa kwa hata baadhi ya mikoa ambayo imekuwa haisikiki katika medani ya soka kuamka kutokana na kuunda timu ambayo inauwakilisha mkoa katika michuano hiyo.
Aidha michuano yab kombe la Taifa, inatumika pia kuleta umoja, ushirikiano na upendo sambamba na burudani ambayo baadhi ya mikoa imekuwa ikiikosa kutokamna na kukosa kushuhudia michuano mbalimbvali na hasa ya ligi kuu bara.
Chini ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) michuano hiyo imekuwa ikifanyika  na kuna nyakati imeshindwa kufanyika kutokana na sababu mbali mbali na hasa kukosekana kwa wadhamini wa michuano hiyo.
Mara ya mwisho michunao hiyo ilifanyika mwaka 2011 ambapo kampuni ya bia Tanzania (TBL) ilikuwa ikiidhamini michuano hiyo kupitia vinywaji vyake tofauti kuanzia mwaka 2005.Mara ya mwisho ilifanyika mwaka 1994.
Hata hivyo, mpaka sasa TFF imeshindwa kabisa kufanya jitihada zozote za kuhakikisha michuano hiyo inarejea tenja ili kurejesha hadhi ya kabumbu hapa nchini.
Kwamba, kuna  mikoa  ambayo haina timu zinazoshiriki Ligi Kuu  mfano mkoa wa Singida ‘Kindai United’uliotwaa ubingwa huo mwaka 2010, iliweza kutoa upinzani mkubwa na hata kutwaa kombe.
Kama hiyo haitoshi hata katika usajili wa wachezaji kulikuwa na ushindani wa hali ya juu kama usajili wa ligi kuu bara ambako baadhi ya wachezaji walijikuta wakigombaniwa na mikoa zaidi ya mmoja na mwisho wa siku suala la kucheza wapi lilibaki kwa mchezaji.
Raha ilikuwa kwa timu ya mkoa wa Dar es Salaam ‘Mzizima United’  katika usajili kusheheni nyiota wengi wanaocheza ligi kuu bara na hasa Simba na Yanga, kabla ya baadaye kugawanywa katika mikoa mitatu yaani Temeke, Ilala na Kinondoni.
Kupitia michuano hiyo ambayo ilikuwa na msisimko wa aina yake, tulipata kuona ushindani wa hali ya juu toka kwa timu shiriki ambapo kila mkoa ulijitahidi kusajili wachezaji wazuri ambao waliweza kutoa ushindani mkubwa kwa timu pinzani.
Kwa vile michuano hiyo ilikuwa inafanyika kipindi ambacho ligi imesimama, baadhi ya vilabu pia viliitumia kupata wachezaji ambao iliwasajili katika vilabu vyao.
Kwa mantiki hiyo, tangu kusimama kwa michuano hiyo hamasa ya soka imekosa msisimko zaidi imebakiki kwa mechi za Simba na yanga tu kidogo na timu ya Taifa.
Hivyo  ni vema kwa TFF kufanya kila liwezekano kwa kuongea na makampuni makubwa  ambayo yataweza kusaidia kufanyika kwa  michuano hiyo kwa mara nyingine na  fursa  kwa  wadau wa soka mikoani kupata burudani ya aina yake.
Hawa ndio mabingwa wa Taifa Cup  Pwani ( 1964), Tanga (1965), Kilimanjaro (1966), Pwani (1967, 1968), Tanga (1969), Morogoro (1970), Kilimanjaro (1971), Pwani (1972),Tanga (1973), Morogoro (1974)Dar es Salaam (1975,1976,1977), Kilimanjaro (1981,1983), Mwanza (1984,1985), Dar es Salaam (1986,1987,1998).

Mwak 1999 hadi 2004 haikufanyika kabla ya mwaka 2005 Mbeya kuwa bingwa, 2006/2007 bingwa alikuwa Dar es Salaam, Ilala (2008, 2009), Singida (2010) na Mbeya  (2011).

YANGA MDHARAU MWIBA.....

$
0
0
Na Dina Ismail

KUNA usemi  maarufu ‘Mdharau mwiba, mguu huota tende!

Huu msemo una maana kubwa sana na ni wajibu kuutilia maanani.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara, Yanga Sc kwa leo ndio walengwa wa msemo huu.

Kwa miezi kadhaa sasa hali ya kiuchumi ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya jangwani na Twiga imekuwa si nzuri.

Hiyo inatokana na mwenyekiti wake ambaye pia ni mfadhili wa klabu hiyo, Yussuf Manji kupata misukosuko na serikali.

Kutokana na hali hiyo kuna baadhi ya mambo na hasa yahusianayo na masuala ya kifedha ndani ya klabu hiyo yalianza kuyumba.

Mwezi Machi mwaka huu, Katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwassa alikiri kuwawepo kwa hali mbaya ya kiuchumi kiasi cha wachezaji kutolipwa mshahara wa mwezi mmoja.

 Mkwassa alisema  tangu Manji aingie matatani, hajawahi kufika katika ofisi za klabu hiyo hivyo wamekuwa na wakati mgumu wa kupata fedha za kuendesha klabu na hivyo walikuwa mbioni kuandaa utaratibu wa kuwataka wanachama na wapenzi wa Yanga waweze kuichangia ili iweze kutimiza malengo yake ya kutetea ubingwa wa ligi kuu.

Kama hiyo haitoshi, baada ya siku chache baadae  ilitangaza kuachana na aliyekuwa Mkurugenzi wake wa benchi la ufundi, Mholanzi Hans van der Pluijm kutokana na sababu hiyo.

Ukata huo ulipelekea pia wachezaji kugomea mazoezi kwa siku kadhaa wakishinikizwa kulipwa mishahara yao, kabla ya kuwekwa sawa na kuendelea na maandalizi yao ya ligi kuu bara na michuano ya kombe la Shirikisho.

Wiki iliyopita kumeibuka taarifa za mshambuliaji wake wa kimataifa Mzambia Obrey Chirwa kugoma kufanya kazi ndani ya klabu hiyo hadi alipwe malimbikizo yake ya mishahara ya miezi mitatu.

Chirwa pia alikataa kusafiri na wenzake kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya, Mouloudia Club Alger  uliofanyika Jumamosi Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Algiers ambapo walifungwa jumla ya mabao 4-0 hivyo kuondolewa katika michuano hiyo kwa jumla ya mabao 4-1.

Hali ya ukata ni kitu cha kawaida hasa kwa vilabu vyetu vya bongo lakini je viongozi huwa wanalichukuliaje na hasa kwa vilabu vikubwa ambavyo vinakuwa katika harakati muhimu.

Mpira ni ajira yao wachezaji kwani kuna wenye familia ambazo zinawategemea hivyo kama wasipolipwa stahiki zao ni lazima watashindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo.

Ni bora ya chirwa ambaye ameamua kujilipua mwenywe ili kufikisha salamu kwa uongozi kuliko hao waliokaa kimya sababu hamjui wanapanga nini vichwani mwao.

Yanga inakabiliwa na mchakamchaka wa kuwania ubiongwa pamoja na michuano ya kombe la Shirikisho hivyo ni kipindi ambacho wachezaji walipaswa kulipwa vizuri ili kuwekeza nguvu katika michuano hiyo.

Lakini kwa sasa akili zao zitakuwa zikiwaza fedha tu na matokeo yake timu itajikuta inafanya vibaya katika michezo yake na kuanza kumtafuta mchawi wakati wanajiroga wenyewe.

Yanga ni timu kubwa, timu pendwa  yenye mashabiki wenye hadhi na madaraja tofauti  katika ukanda wa Afrika  mashariki na Kati ambao wakiamua wanaweza kuichangia klabua yao ili kulipa mishahara ya wachezaji na shughuli nyingine za klabu.

Kinachoonekana ni mawasiliano duni baina ya uongozi wa klabu na wadau wake kwani naamini kuna matajiri wengi sana ambao wanaweza kuokoa jahazi, lakini uongozi umeamua kumuachia mzigo huo manji pekee tu kitu ambacho sio sahihi kabisa licha ya kuwa ni mfadhili wao.

Hivyo ni wakati wa viongozi kuamka na kutafuta njia mbadala ya kukabiliana na hali hiyo ili kuhakikisha wachezaji wanapata stahiki zao na kazi ibaki kwao kutimiza wajibu wao uwanjani.

Kwa kuacha hali ibaki hivyo hivyo mwisho wa siku itawagharimu maana leo kaanza Chirwa, kesho atakuja Tambwe  (Hamis), na mwisho wa siku timu nzima, sasa ikifikia huko unadhani timu itakuwa na mafanikio tena?


Kauli mbiu ya  Yanga ‘Daima Mbele nyuma Mwiko’ nadhani ndio ifuatwe kwa kuweka sawa kasoro ndogondogo kama hilo suala la mishahara ili baadae wasije patwa na Matende!

VILABU VIWE WAZI KATIKA USAJILI WA WACHEZAJI

$
0
0
Na Dina Ismail

NI kawaida kwa vilabu vya soka ndani na nje ya nchi kufanya usajili kwa ajili ya wachezaji itakoawatumia katika ligi na michuano mbalimbali.

Mara nyingi usajili hufanywa mara mbili, yaani kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi na kabla ya kuanza kwa  raundi ya pili ya ligi.

Kwa vipindi hivyo tumekuwa tukisikia tetesi ama kauli za wazi kutoka kwa viongozi wa vilabu husika kuhusiana na wachezaji wanaosajiliwa ama kuachwa katika vilabu husika.

Kwa Tanzania bado tuko nyuma katika suala la usajili na zoezi hilo hufanywa kisiasa, kisanii na kibabe zaidi kitu ambacho sio kizuri katika maendeleo ya soka letu.

Kwamba, kipindi cha usajili kinapofika badala ufanyike usajili wa kitaalam zaidi, unafanyika usajili kwa ajili ya kutimiza wajibu tu.

Hii ina maana kwamba, suala la usajili inabidi lifanywe na mkuu wa benchi la ufundi yaani kocha ambaye hupendekeza majina ya wachezaji au nafasi ambazo zinahitaji kujazwa, pia wachezaji ambao hawahitaji katika timu.Hapo kazi inabaki kwa uongozi kutimiza kile alichikitaka kocha!

Lakini kwa hapa nchini utaratibu huo haufanyiki kwa asilimia kubwa, kinachofanyika hapo ni ujanja ujanja tu, kwani utakuta kila kiongozi anataka mchezaji wake asajiliwe au upande mwingine kuna viongozi wanataka fulani aachwe wakati kocha anamuhitaji kundini.

Sasa huko ni kuingilia uhuru wa kocha kwani mwisho wa siku timu inajikuta inasajili au inabaki na wachezaji ambao si changuo la kocha hivyo timu itakapofanya vibaya, jumba bovu linamuangukia kocha.

Kocha ni mtaalamu hivyo maamuzi yake hayana budi kuheshimiwa, kinyume na hapo timu itajikuta kila mwaka inabadili makocha, pia kutumia fedha nyingi kila msimu kwa ajili ya usajili, hapo hapo kutopata matokeo mazuri.

Suala jingine ambalo vilabu vya Tanzania vinachemsha kwa upande wa usajili ni uwazi katika mchakato wa zoezi hilo, yaani wenzetu waliopiga hatua wako vizuri kwa kutangaza wazi nyota ambao haitawahitaji baada ya kuisha kwa msimu.

Kutangaza nyota unaowatema mapema ni jambo zuri kwani utatoa nafasi kwa mchezaji kuwa na utayari wa kujijua kwamba hatokuwa katika kikosi hicho hivyo aanze mchakato wa kusaka timu.

Pia kutanngaza mapema wachezaji unaowaacha kutatoa fursa kwa timu nyingine pia kufanya nao mazungumzo kwa ajili ya kuwasajili kwa sababu sio wachezaji wote wanaotemwa ni wabovu!

Lakini cha kushangaza, suala la usajili hufanywa siri sana na hasa wachezaji wanaoachwa na mwisho wa siku zoezi linapofungwa wachezaji walioachwa kujikuta hawana kazi tena kwa msimu mzima.

Kwamba, kipindi cha usajili kimefungwa na klabu ndio inatangaza kuwa imemuacha fulani,sasa hapo unakuwa umempotezea mwelekeo wake sababu mpira ni ajira yake hivyo itabidi aishi maisha ya kubangaiza mpka msimu mpya wa ligi.

Nadhani ifikie wakati kwa vilabu kubadilika kwa kufanya usajili kulingana na Sayansi na Teknolojia.



SAPOTI KUBWA KWA TIMU YA TENISI KWENYE KOMBE LA DUNIA

$
0
0
Na Dina Ismail

KWA muda mrefu Tanzania tumekuwa wasindikizaji katika michezo mbalimbali na hasa katika ngazi ya kimataifa.

Licha ya kuwepo kwa wachezaji wengi wenye vipaji katika michezo husika lakini tumejikuta tukiishia njiani katika harakati za kusaka tiketi ya kucheza kombe la dunia.

Bahati nzuri tumekuwa tukipata nafasi za kushiriki katika kuwania kucheza mashindano mbalimbali ya dunia lakini tumekuwa tukiishia njiani tu na hata tukibahatisha tunatolewa mapema.

Hivi karibuni timu ya Taifa ya Tenisi kwa watu wenye ulemavu imeweza kuitoa kimasomamso Tanzania baada ya kufuzu kucheza  mashindano ya kombe la dunia kwa mchezo huo.

Timu hiyo ilifuzu hatua hiyo bada ya kushika nafasi ya kwanza  katika michuano ya Afrika iliyofanyika Nairobi, Kenya  na hivyo itaiwakilisha Afrika katika mashindano ya Dunia yatakayofanyika nchini Italia mwezi Mei mwaka huu.

Ni hatua kubwa na ya kupongezwa kwa timu hiyo pia ni  jambo la kujivunia  kwani  pamoja na kudaiwa kufanya maandalizi katika mazingira magumu lakini waliweza kukabiliana na changamoto walizokutana nazo na hatimaye waliweza kushinda.

Kocha wa timu hiyo, Riziki Salum alikaririwa na vyombo vya habari akizungumzia changamoto  mbalimbali walizokumbana nazo  katika mashindano hayo lakini hawakukata tamaa na kuhakikisha wanaitoa kimasomaso Tanzania na Afrika kwa jumla.

Riziki alieleza kwamba walikuwa wakifanya mazoezi na maandalizi yao katika mazingira magumu lakini wachezaji wake waliweza kukabiliana na hali hiyo na kufanya kile walichodhamiria na matokeo yake waliweza kushinda.

Hivyo basi ni wakati kwa wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia timu hiyo kwa hali na mali kuhakikisha inafanya vema katika michuano ya kombe la dunia na kuitoa kimasomaso Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Kwamba, jukumu la kuisaidia timu hiyo lisiachwe kwa viongozi tu wa chama husika bali liwe kwa kila mwenye nafasi ya kuchangia kufanya hivyo kwani hawa ni wawakilishi wa Tanzania na si chama binafsi.

Ifikie wahakati tuachane na kasumba ya kuthamini michezo kama soka au mpira wa kikapu tu kwa kuipa sapoti kubwa  pindi inaposhiriki mashindano mbalimbali huku michezo mingine ikidharaurika na wachezaji kuachwa kama watoto yatima.

Fikiria timu kama hiyo ya watu wenye ulemavu, kwa hali iliyokuwa nayo klakini imeweza kupambana kadiri ya uwezo wake na kuweza kushinda timu nyingine ambazo zilikuwa na sapoti kubwa toka kwa wananchi na viongozi wake.

Hiyo ni timu ya Watanzania wote na itakuwa fahari sana kama itaenda huko na kufanya vema na kuitangaza vema nchini.


Yaliyopita si ndwele tuanze sasa kwa timu hiyo na tusisubiri kuja kuipokea na kuandalia dhifa kubwa, kuialika bungeni  au Ikulu kama itatwaa ubingwa wa dunia wakati walihangaika peke yao katika maandalizi.

SIMBA CHEZENI MPIRA ACHENI KULIALIA

$
0
0
Na Dina Ismail

SIMBA  imejikuta ikihaha kupigania mabao matatu na pointi tatu ilizopokwa na  kamati  ya Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Vinara hao wa ligi kuu walikata rufaa kwa kamati ya usimamizi na uendeshaji wa Ligi Tanzania ‘kamati ya masaa 72’ ikidai Kagera Sugar kumchezesha beki mohammed Fakhi  wa Kagera Sugar wakati akiwa ana kadi tatu za njano.

Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Kaitaba mjini Bukoba  Aprili 2 mwaka huu, Simba ililala kwa mabao 2-1.

Kwamba, kamati ya masaa 72 iliipa mabao matatu na pointi tatu  Simba baada ya kujiridhisha kwamba  Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano.

Hata hivyo Kagera Sugar ilipinga na kukimbilia kamati ya katiba Sheria na Hadhi wachezaji  kabla ya kamati hiyo kuamua kuipoka ushindi huo wa mezani Simba baada ya kugundua kuwepo kwa makosa kadhaa katika kuipa ushindi wa mezani Simba.

Selestine Mwesigwa, Katibu Mkuu wa TFF akizungumzia hatua hiyo alibainisha mambo kadhaa yaliyopelekea kubatilishwa kwa maamuzi hayo ikiwemo Simba kutowasilisha kwa wakati na hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 20 kifungu cha kwanza cha kwanza cha kanuni za Ligi Kuu toleo la mwaka 2006 inayotaka malalamiko yote yawasilishwe kwa maandishi Bodi ya Ligi siyo zaidi ya saa 72 baada ya mchezo kumalizika kwa mchezo.

Pili, Mwesiga alisema  malalamiko hayo hayakulipiwa ada kwa mujibu wa kanuni ya 20 kifungu cha nne kinachosema ada ya malalamiko ni Sh. 300,000 na kwamba malalamiko yatakayowasilishwa bila kulipiwa ada au baada ya muda uliowekwa hayatasikilizwa.

Sababu ya tatu aliyoitaja Mwesigwa ni kwamba kikao cha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania, maarufu kama Kamati ya Saa 72 kilikosa uhalali baada ya kuwashirikisha Wajumbe waalikwa ambao siyo sehemu ya Kamati hiyo.

Maamuzi hayo yameonekana kuichanganya sana Simba na hivyo kuwa na mikakati ya kuhakikisha inapanda ngazi za juu zaidi ili kuweza kudai haki yao.

Nadhani Simba ingeachana na hili suala na kuelekeza nguvu zake katika michezo yake ya Luigi ambayo imebakiza wiki chache kabla ya kumalizika.

Kwamba, inawezekana ni kweli wana haki lakini walifanya makosa wenyewe katika hatua za awali za kukata kwao rufaa kwa kukosea baadhi ya kanuni na taratibu zilizopo katika katika ya TFF kama kama alivyoeleza Katibu Mkuu wa TFF

Hivyo basi kuendelea kufuatilia suala hilio ni kupoteza muda kwani nguvu inayotumika katika zoezi hilo ni bora ingeelekezwa katika maandalizi ya michezo iliyonayo timu hiyo ambayo kwa sasa inaongoza Ligi hiyo  ikiwa na pointi 59, huku mabingwa watetezi Yanga wakishika nafasi ya pili kwa pointi 56.


Sote tunafahamu Simba imepania kutwaa ubingwa wa Bara msimu wa 2016/2017 baada ya kuukosa kwa miaka zaidi ya mitano hivyo ni vema ikajiongeza kwa kupata ushindi wa halali badala ya kubaki inaililia pointi za bure.

MISS TANZANIA ZAIDI YA SHINDANO, LIMEWATOA WENGI

$
0
0
Na Dina Ismail

MIAKA ya nyuma  shindano la Miss Tanzania lilikuwa likichukuliwa kama uhuni  kiasi cha wazazi kukataza watoto wao kushiriki.

Lakini kadiri miaka ilivyosonga ndipo wazazi walianza kulikubali shindano hilo kwa kuruhusu watoto wao baada ya kuona mafanikio waliyoyapata baadhi ya warembo mara baada ya kushiriki shindano hilo.

Miss Tanzania ‘beauty with purpose’ ni zaidi ya shindano kwani mrembo anaweza asishinde taji kuu lakini akanufaika kutokana na ushiriki wake.

Kwa mantiki hiyo kuna baadhi ya wadada ambao walipata kushiriki shindano hilo leo hii wamejijengea heshima kubwa katika jamii kutokana na kazi wanazozifanya, lakini heshima inaanzia kushiriki kwao Miss Tanzania.

Kihistoria shindano hilo kwa hapa nchini lilianza rasmi mwaka 1960 na mrembo wa kwanza kutwaa taji hilo alikuwa Theresia Shayo ambaye sasa hivi ni marehemu.

Hata hivyo kutokana na maadili na utamaduni wa Tanzania serikali ililifuta mwaka 1967 kabla ya kurejeshwa tena katika miaka ya 1990 na ndipo hapo Tanzania ilianza kupata mafanikio kupitia mashindano ya urembo.

Mrembo  Aina Maeda ndiye alikuwa mrembo wa kwanza tangu kurejeshwa kwa mashindano hayo ambapo alitwaa taji hilo mwaka 1994 yakiwa chini ya uratibu wa Hashim Lundenga.

Mashindano hayo yalianza kwa kuendeshwa kimkoa na kadiri miaka ilivyosogea wigo wake ulitanuka na kufikia kufanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara, wilaya, vitongoji  na hata katika ngazi ya vyuo vya elimu ya juu kulisakwa washiriki.

Kupitia mashindano hayo, pamoja na zawadi nono za nyumba, magari pamoja na mamilioni ya fedha, tumeshuhudia warembo mbalimbali wakijipatia umaarufu ambao uliwawezesha kupata kazi katika makampuni mbalimbali, mikataba katika makampuni mbalimbali ya matangazo na mengine mengi.

Hawa ni baadhi ya warembo waliopitia Miss Tanzania na sasa hivi wanaheshimika kutokana na kazi wanazozifanya sambamba na mchango wao mkubwa katika jamii:

Hoyce Temu:

Huyu ni Miss Tanzania mwaka 1999 ni mrembo ambaye amekuwa mfano wa kuigwa kwa  kufanya zaidi shughuli za kijamii   kwani tangu atwae taji hilo jina lake limebaki kuwa juu kila uchwao.

Mrembo huyo licha kipindi chake cha mwaka mmoja cha kufanya kazi za kusaidia jamii kama Miss Tanzania lakini ameendelea kuifanya hivyo hadi sasa  ambapo kupitia kipindi chake cha Televisheni cha ‘Mimi na Tanzania’ amekuwa akiongea na watu wenye shida mbalimbali na kuwaombea misaada kwa wasamaria.

Hoyce ambaye kwa sasa anafanya kazi kitengo cha mawasiliano na Mahusiano katika ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) nchini Kwa kutambua huduma yake kwa jamii, aliwahi kutajwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga kama mlimbwende bora kuliko wote.

Nancy Sumari:

Alitwaa taji la Miss Tanzania 2005, pia taji la Miss World Afrika mwaka huo.

Ni mrembo mwingine msomi na anayeheshimika hapa nchini kutokana na utumishi wake katika jamii.

Nancy ni mfanyabiashara, pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bongo Media, pamoja na Mfuko wa  The Neghesi Sumari Foundation.Pia ni mtunzi wa kitabu cha hadithi za watoto kiitwacho, Nyota Yako.

Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K-Lyn’:

Ni mrembo aliyetwaa taji mwaka 2000.Kabla ya kushiriki shindano alikuwa akijihusisha na uimbaji wa muziki katika bendi ya Tanzanite.

Baada ya kumaliza kulitumikia taji lake aliendelea kuwa msanii ambako alitoa singo zake kama msanii wa kujitegemea huku vibao vyake kama Crazy Over You, Nipe mkono, Best na nyinginezo ambazo zilimpatia umaarufu zaidi.

K-Lyn ambaye ni mke wa mfanyabiasha maarufu nchini Reginald Mengi kwa sasa amejikita zaidi katika biashara akimiliki duka la liitwalo Amorette ambalo linatengeza na kuuza thamani za ndani pamoja na upambaji wa ndani.

Jokate Mwegelo:

Jina lake lilianza kusikika zaidi mwaka 2006 aliposhika nafasi ya pili katika shindano la Miss Tanzania, huku taji hilo likitwaliwa na Wema Sepetu.

Jokate alitwaa taji la balozi wa kinywaji cha Redd’s kilichokuwa mmoja ya wadhamini wa shindano hilo ambapo aliweza kufanya kazi mbalimbali zilizohusiana na mitindo na ubunifu kama balozi.

Baada ya muda wake kumalizika Jokate alionekana kupenda zaidi masuala ya mitindo ambapo alijikita katika sekta hiyo, sambamba na kujihusisha na uigizaji na muziki.

Kwa sasa Jokate amejikita zaidi katika biashara chini ya Lebo yake aliyoipa jina la Kidoti ambapo ameshaingiza sokoni bidhaa zake kadhaa ikiwemo nywele, mabegi ya shule na kandambili.

Aidha, mrebo huyo pia anaendesha kampeni yake iitwayo ‘Be Kidotified’ inayohamasisha wanafunzi wenye vipaji mbalimbali kutojiweka nyuma.


Happiness Magesse ‘Millen’:

Jina lake linang’ara duniani kwa sasa kupitia fani ya mitindo.

Alitwaa taji la Miss Tanzania mwaka 2001 na baada ya kumaliza muda wake alikwenda nchini Afrika Kusini na kuanza kujihusisha na kazi ya mitindo ambayo anaifanya mpaka sasa.

Millen ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani pia anamiliki mfuko wake uitwao ‘Millen Foundation’ ambao ni mahususi kwa kuendesha kampeni maalum ya kuelimisha wasichana juu ya ugonjwa wa Endomitriasis ambao huwasababishia maumivu makali wakati wa siku zao za hedhi.


Hao ni baadhi kwani wapo warembo wengi tu  waliopitia katika shindano hilo ambao wanafanya mambo makubwa ya kueleweka katika jamii.


SINGIDA UNITED, LIPULI NA NJOMBE FC JIPANGENI MSIISHIE KUSINDIKIZA VPL

$
0
0

Na Dina Ismail

LIGI kuu soka Tanzania bara  inaelekea ukingoni ambapo  mshike mshike upo katika makundi mawili, zile zinazowania ubingwa wa msimu wa 2016/17 na zenye kupambana na kushuka daraja.

Katika mbio za kuwania ubingwa, vigogo vya soka nchini Simba na Yanga ndizo zinazopambana kuwania ubingwa wa ligi hiyo, huku Majimaji, Toto Africans,JKT Ruvu na Mbao Fc zikiwa katika mchuano wa mojawapo kujikwamua kubaki Ligi kuu kwani timu tatu za mwisho zitashuka.

Msimu mpya wa ligi 2017/2018 utazikaribisha timu za Singida United (Singida), Lipuli Fc  na Njombe mji zote kutoka mkoani Iringa ambako timu hizo kwa sasa zimeshaanza maandalizi kwa na namna moja ama nyingine.

Singida United na Lipuli Fc si mara yao ya kwanza kushiriki katika ligi hiyo ambako mara ya mwisho zilishiriki ilikuwa miaka 17 iliyopita na kisha kushuka daraja.

Njombe mji yenyewe yenye maskani yake katika mji wa Njombe mkoani Iringa hii itakuwa mara yake ya kwanza kushiriki katika ligi kuu.

Kwa wanaofuatilia historia ya soka la bongo na hasa Ligi Kuu ni wazi kwamba wanazifahamu sana Singida United na Lipuli na hiyo inatokana na umahiri wao ilizokuwa nazo enzi zinashiriki ligi hiyo.

Tuseme ni bahati mbaya tu kwao ilipelekea kushuka daraja lakini  ni timu ambazo zilikuwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu kiasi ambacho vigogo vya soka nchini Simba na Yanga ziliweza kuvuna wachezajaji kutoka huko kwa nyakati tofauti.

Kwa sasa timu hizo zipo katika maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu na ili kuweza kushiriki vyema tayari zimeanza mikakati madhubuti ya kuimarisha vikosi v yake, benchi la ufundi na miundombinu yake, yaani viwanja vya mazoezi.

Timu ya Singida United kwa kuonesha kuwa imejipanga vema kushiriki kikamilifu tayari imefanya maboresho kwenye benchi lake la ufundi kwa kumuajiri aliyepata kuwa kocha na Mkurugenzi wa benchi la Yanga, Hans Van Der Pluijm.

Kama hiyo haitoshi, Singida United pia imeanza usajili wake kwa kuwasajili wachezaji watatu wa  kimataifa kutoka Zimbabwe, Tafadzwa Kutinyu, Elisha Muroiwa   na Wisdom Mtasa.

Singida United pia ipo katika ukarabati wa hali ya juu wa Uwanja wa Namfua ambao itautumia katika ligi hiyo kama uwanja wake wa nyumbani.Zoezi hilo linafanywa na Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida.

upandaji wa nyasi huku ikielezwa ifikapo Agosti mechi zote za nyumbani zitachezwa uwanjani hapo.

Singida United ambayo imemwajiri kocha mpya Mholanzi, Hans Pluijm  na kusajili wachezaji watatu wa kigeni ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda daraja kushiriki ligi kuu msimu ujao pamoja na Njombe Mji na Lipuli FC.

Kwa upande wa Lipuli Fc, ambayo iko chini ya Chama cha soka Mkoa wa Iringa (IRFA) iliyochukua jukumu la kuiendesha klabu hiyo kutokana na  kuwepo kwa  mgogoro uliozuka ndani ya uongozi wa klabu hiyo,nayo ipo katika mipango ya kujiweka sawa ili kushiriki vema katika ligi hiyo.

Njombe Mji Fc ambayo inanolewa na kocha maarufu nchini, Hassan Banyai nayo imedhamiria kuhakikisha inashindana na si kushiriki kwenye ligi hiyo kubwa nchini.

Kwa mantiki hiyo, timu hizo zitacheza ligi hiyo kiushindani zaidi na si kufanya bora liende na hasa ikizingatia zilifanya juhudi na jitihada kubwa kuhakikisha zinapanda hadi ligi hiyo.

Kwamba, ziwe mfano kwa timu nyingine zinazopanda kwa kufanya vema na hata ikiwezekana mojawapo itwae ubingwa au hata kuingia tatu bora mwishoni mwa ligi.

Ushiriki wao usiwe nguvu za soda kwa kuishia kuzifunga tu Simba na Yanga halafu mechi nyingine zinapoteza, zitakuwa zimewakosea sana wananchi na pia kupoteza nguvu, heshima na jitihada bure za wakazi wa miji ya Iringa na Singida ambao walikuwa nazo bega kwa bega mpka zinapanda.


Aidha, ni vema timu hizo zikajiepusha na siasa za Simba na Yanga, kuanzia katika usajili na hata kipindi watakachoanza kushiriki Ligi Kuu, zicheze soka la ushindani kama zilivyofanya katika Ligi daraja la kwanza.

YANGA YAAJIRI VIONGOZI WAPYA 4

$
0
0

KLABU ya Yanga imeajiri maofisa wanne wapya,ambao ni Khamis Jecha,Jimmy Kindoki ( Idara ya Wanachama na Mashabiki),Willy Shemoka (Idara ya Habari na Mawasiliano) na Ibrahim Samuel ( Mkurugenzi wa Idara ya Masoko)

STARS YAANZA VIBAYA AFCON,YATANDIKWA 3-0 NA MOROCCO

$
0
0

TAIFA Stars  imeanza vibaya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kutandikwa mabao 3-0 na Morocco katika mchezo wa Kundi F uliopigwa  usiku huu Uwanja wa Uwanja wa Laurent Pokou Jijini San-Pedro, Ivory Coast. 

Katika mechi hiyo Stars  ilimaliza pungufu baada ya kiungo wa  Novatus Dismas Miroshi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 70 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.

Morocco ilijipatia mabao yake kupitia na beki  Romain Ghanem Paul Saïss , kiungo  Marseille  Azzedine Ounahi na mshambuliaji na Youssef En-Nesyri.

MEXIME AWAPIGA MKWARA WACHEZAJI WAKE

$
0
0

 Kocha Mkuu wa Ihefu FC, Mecky Maxime  amewataka wachezaji wake kutumia vipaji vyao ipasavyo ili kuipa matokeo mazuri timu hiyo.

Maxime alisema nafasi waliyopo kwenye msimamo haiendani na ukubwa wa majina na umaarufu waliokuwa nao wachezaji wake

“Ligi ya msimu huu ni ngumu inahitaji wachezaji wanaopambana na siyo umaarufu au ukubwa wa majina mimi na vijana wangu tunapaswa kupambana na kila mmoja kutimiza wajibu wake   ili kuiondoa timu kwenye nafasi mbaya iliyopo hivi sasa,” alisema Maxime.

Aliongeza kuwa  usajili walioufanya kwenye dirisha dogo ni mzuri na unakwenda kuwaongezea nguvu lakini kitu cha kwanza lazima kila mtu atimize jukumu lake la msingi.

Aliongeza kuwa na wachezaji wazuri wazuri siyo kitu muhimu sana kama wachezaji hao hawajitumi hivyo atahakikisha anaanda mpango mkakati maalumu utakaomwezesha kila mchezaji kuchangia mafanikio waliyoyakusudia.

Ihefu iliyopo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu   imefanya usajili mkubwa kwenye dirisha dogo baadhi ya wachezaji iliyo wasajili ni Elvis Rupia, Duke Abuya na Bruno Gomes wote kutoka Singida Fountain Gate 

GAMONDI AMTABIRIA MAKUBWA GUEDE

$
0
0

KOCHA MKuu wa Yanga, Miguel Gamondi amemtabiria makubwa mshambuliaji mpya wa timu hiyo Joseph Guede akisema atawasaidia sana  kutetea mataji yote ya ndani.

Yanga ilifunga dirisha dogo la usajili juzi kwa kumtambulisha Guede raia wa Ivory Coast kama mrithi wa Hafidh Konkoni ambaye kiwango chake hakikumvutia kocha huyo raia wa Argentina.

Gamondi  alisema kupata saini ya mshambuliaji huyo ni sawa na kumaliza tatizo sugu la umaliziaji ambalo limemsumbua tangu aichukue timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu.

“Naujua vizuri uwezo wa Guede, ni mshambuliaji aliyekamilika anajua kufunga lakini hata kutengeneza nafasi kwa wenzake binafsi imani yangu nikubwa kwake kitu cha msingi kwake ni kuthibitisha hilo kwa kufunga mabao yakutosha,” alisema Gamondi.

Licha ya uzoefu mkubwa aliokuwa nao kutokana na kucheza ligi mbalimbali Afrika na Ulaya,Gamondi  amemtaka mchezaji huyo kupambana uwanja wa mazoezi ili kugombea nafasi ya kucheza na washambuliaji waliopo.

Alisema yeye ni kocha anayetenda haki hivyo pamoja na rekodi nzuri alizokuwa nazo kama atashindwa kujituma atamweka nje na kuwapa nafasi wachezaji wengine ambao watakuwa wanafanya vizuri mazoezini.

Guede ( 29),amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miezi sita akitokea timu ya Tuzlaspor FC ya Uturuki.


TANZANIA YAJIFUNZA MAANDALIZI YA AFCON 2027 KUTOKA IVORY COAST

$
0
0

 


Na Brown Jonas – WUSM, Ivory Coast

WAZIRI  wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro ametembelea Uwanja wa Mpira wa Miguu  wa Laurent Pokou uliopo jijini San Pedro nchini Ivory Coast ili kujifunza na kuona  namna ambavyo nchi hiyo imefanya maandalizi ya uenyeji wa AFCON 2023 ikiwemo ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya mashindano hayo makubwa Afrika.

Dkt.Ndumbaro amefanya ziara hiyo sanjari na kuhudhuria mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon2023) yanayoendelea nchini humo kama sehemu ya Tanzania kuendelea kujiandaa na  uenyeji wa  mashindano hayo mwaka 2027 kwa kushirikiana na Kenya na Uganda.  

Dkt. Ndumbaro amesema aina ya uwanja aliouona  unafaa pia katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo amesema Serikali mbali na kuendelea kujenga viwanja vya michezo Dodoma na Arusha inaendelea kukaribisha wadau wengine kuunga mkono juhudi hizo katika ujenzi wa miundombinu ya michezo katika mikoa mingine.  

Katika ziara hiyo,Dkt. Ndumbaro ameambatana na Kaimu Balozi wa Kituo cha Abuja anayehudumia pia nchi ya Ivory Coast, Judika Nagunwa, Kaimu Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo  Ally Mayay na maafisa wengine wa wizara.

MWAKINYO ACHAGIZA MAPRO

$
0
0

 BONDIA Hassan Mwakinyo amesema mapromota wanaotaka kumewekea gari kwa ajili ya pambano milango iko wazi.

Mwakinyo aliandika ujumbe huo jana kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii akisema sasa yuko tayari kwa mapromota wanaotaka kumewekea gari kwa ajili ya kupigana kama zawadi.

“Haya sasa mapromota anayetaka kuniwekea gari milango iko wazi,”ulisomeka ujumbe huo huku akiwa ameweka picha ya gari kuonesha umuhimu wake.

Haitakuwa mara ya kwanza hapa nchini kwa bondia kupigana kwa ushindi wa gari kwani bondia kutoka Morogoro Twaha Kassim ‘Kiduku’ aliwahi kupigana na kushinda gari aina ya Toyota Crown mwaka juzi.

Mwakinyo kwa sasa anajiandaa na pambano la usiku wa Mtata Mtatuzi litakalopigwa Januari 27 mwaka huu kwenye Uwanja wa New Amaan Zanzibar dhidi ya bondia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mbiya Kanku kuwania mkanda wa dunia wa WBO.


LOMALISA 'AJIFUNGA' MMOJA TENA YANGA

$
0
0

 BEKI wa kushoto wa Yanga, Joyce Lomalisa ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Mkataba wa awali wa beki huyo unamalizika mwishoni mwa msimu huu hivyo uongozi kwa kushirikiana na benchi la ufundi umeamua kumuongeza mwaka mmoja kutoka na kuvutiwa na huduma yake.

Lomalisa alisema kilichomfanya kukubali kuongeza mkataba mpya ni malengo waliyokuwa nayo viongozi wa timu hiyo hasa katika mashindano ya kimataifa.


“Yanga ni sehemu salama kwangu viongozi wake wana maono ya mbali ndiomaana nimechagua kubaki hapa naamini nitafika mbali zaidi hasa katika mashindano ya kimataifa,” alisema Lomalisa.

Beki huyo alisema katika kipindi cha misimu miwili ambacho ameichezea timu hiyo amebaini mambo mengu mazuri ikiwemo kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita na kubeba ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la FA.

Alisema kwa sasa akili na mawazo yake ameyaweka kwenye klabu hiyo kuhakikisha anashirikiana na wenzake ili kuipa mafanikio zaidi katika mashindano yote ambayo wanashiriki msimu huu.

Lomalisa alijiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili mwanzoni mwa msimu huu akitokea Petro Atletico ya Angola na tangu ajiunge amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha kocha

TFF YAMPUMZISHA AMROUCHE,MOROCCO NA MGUNDA WAKABIDHIWA TIMU

STSRS,ZAMBIA ZAGAWANA POINTI AFCON

$
0
0


 TIMU  ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo  imelazimisha sare ya bao  1-1 dhidi ya Zambia katika mchezo wa Kundi F kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Stars ilitangulia kupata bao hiko kupitia shuti kali  la Simon Msuva katika dakika ya 11 bao ambalo lilizipeleka mapumziko timu hizo kwa Stars kuingoza 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kucheza kwa tahadhari kubwa  kabla ya Patson Daka kusawazisha katika  88 kwa mpira wa kichwa. 

Kwa matokeo hayo yanaifanya  Tanzaia kuendelea kushika mkia katika kundi F kwa kuwa na pointi moja ambapo Morocco inaongoza ikiwa na pointi 4, ikifuatiwa Zambia (2) na  DR Congo (2).

Michezo iliyosalia itapigwa keshokutwa  Jumatano Januari 24, 2024 ambapo Tanzania itakipiga na  DR Congo na Zambia itakwaana na Morocco



Latest Images