Quantcast
Channel: Sports Lady
Viewing all 454 articles
Browse latest View live

KAMATI YA MASHINDANO TFF KUKUTANA KESHO KUPITIA MAANDALIZI YA KLABU BINGWA YA MIKOA

$
0
0

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inakutana Jumapili (Mei 5 mwaka huu) kupitia maandalizi ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) iliyopangwa kuanza Mei 12 mwaka huu.
Tayari mikoa 18 kati ya 27 kimpira imeshapata mabingwa wao kwa ajili ya RCL itakayotoa timu tatu zitakazopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao (2013/2014).
Kamati hiyo chini ya Uenyekiti wa Blassy Kiondo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF itapokea taarifa ya maandalizi ya ligi hiyo kutoka Idara ya Mashindano ya TFF na kufanya uamuzi juu ya mikoa ambayo haijawasilisha mabingwa wao.
Ligi hiyo itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini, na ratiba (draw) itapangwa wakati wowote. Ada ya kushiriki ligi hiyo kwa kila klabu ni sh. 100,000 na usajili utakaotumika na ule ule wa ligi ngazi ya mkoa. Hakutakuwa na usajili mpya wa wachezaji. 

KILA LA HERI AZAM FC LEO

$
0
0

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri timu ya Azam katika mechi yake ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika itakayochezwa nchini  Morocco leo.
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano hiyo itachezwa jijini Rabat kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Morocco. Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.
Azam iko nchini Morocco kwa karibu wiki nzima sasa ikijiandaa kwa mechi hiyo chini ya Kocha wake Stewart John Hall. Msafara wa Azam nchini humo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Eliud Mvella.

25 WARIPOTI KAMBI YA YOUNG TAIFA STARS

$
0
0
Wachezaji 25 kati ya 30 walioitwa na Kocha Kim Poulsen kwenye kikosi cha pili cha Taifa Stars (Young Taifa Stars) wameripoti kambini ambapo mazoezi yalianza tangu jana jioni (Mei 2 mwaka huu).
Kocha Kim amewaitaka wachezaji katika kambi hiyo ya siku tano ili kuangalia uwezo wao katika maeneo kadhaa kwa lengo la kupata baadhi ambao anaweza kuwajumuisha kwenye kikosi cha Taifa Stars siku za usoni.

Wachezaji watano walioshindwa kujiunga katika kambi ya timu hiyo iliyoko hoteli ya Sapphire jijini Dar es Salaam ni Aishi Manula, David Mwantika, Himid Mao, Samih Nuhu na Seif Abdallah ambao wako Morocco na timu yao ya Azam.



JAHSON ANAOMBA KURA YAKO TUZO ZA KILI

$
0
0

Mambo vipi watu wangu naomba mnipe tough tunichagua kama mwanamuziki wa ragga nimefanyikisha kuingiza ngoma yangu ya PUSH DEM kwenye kinywang'anyilo cha KILIMANJARO MUSIC AWARD , nipigie kura yako kwa kutumia simu ya mkononi andika BW4 kisha tuma kwenda namba 15345 utakuwa umeniwezesha kushinda tuzo hiyo ahsante tusisahau kula vyakula vya asili kama vile ugali wa mtama na matunda matuna pamoja na mboga za majani 
one love wote
ngoma hii hapa ilioingia kwenye tuzo

https://www.youtube.com/watch?v=6hhDqECILnA

KAMATI YA UTENDAJI TFF KUKUTA MEI 9 KUJADILI UCHAGUZI WAKE

$
0
0

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inakutana Mei 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam kupokea na kupanga utekelezaji wa maagizo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuhusu uchaguzi wa shirikisho.
Kikao hicho cha dharura chini ya Uenyekiti wa Rais wa TFF, Leodegar Tenga kitakuwa na ajenda hiyo moja tu katika kuhakikisha utekelezaji wa maelekezo ya FIFA unafanyika haraka ili uchaguzi ufanyike ndani ya muda uliopangwa.
FIFA katika maelekezo yake imetaka kwanza ziundwe Kamati ya Maadili na Kamati ya Rufani ya Maadili kabla ya kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya TFF. FIFA imeagiza uchaguzi uwe umefanyika kabla ya Oktoba 30 mwaka huu. 

KIPORO CHA SIMBA NA RUVU SHOOTING KULIWA UWANJA WA TAIFA KESHO

$
0
0



Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea Jumapili (Mei 5 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya Ruvu Shooting na Simba itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.15 jioni.
Hiyo itakuwa mechi ya raundi ya 24 kwa timu hizo ambapo Simba iko nafasi ya nne ikiwa na pointi 39 nyuma ya mabingwa Yanga wenye pointi 57, Azam yenye pointi 48 na Kagera Sugar ambayo ina pointi 40. Ruvu Shooting iko katika nafasi ya saba ikiwa na pointi 31.
Hadi sasa mabao 348 yameshafungwa katika ligi hiyo huku Yanga ikiongoza kwa kufunga 45. Polisi Morogoro yenye pointi 22 katika nafasi ya 12 ndiyo iliyofunga mabao machache ikiwa nayo 13 tu.
African Lyon yenye pointi 19 katika nafasi ya mwisho ndiyo inayoongoza kwa kuwa na kadi nyingi. Timu hiyo inayofundishwa na Charles Otieno ina kadi 44 ambapo kati ya hizo nne ni nyekundu. Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani mkoani Morogoro yenyewe inaongoza kwa kuwa na kadi nyingi nyekundu ambapo hadi sasa inazo saba. 

HAFLA YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI NA UZINDUZI WA MFUKO WA MWANGOSI

$
0
0

Mkurugenzi wa MISA-TAN Bw. Tumaini Mwailenge akizungumza na waalikwa kwenye Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa habari Duniani iliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa Mwangosi utakao kuwa ukisaidia waandishi wa habari pindi wapatapo matatizo wakiwa kazini. Kushoto ni Mzee Kassim Mapili wa Mjomba waliosherehesha usiku huo kwa buradani ya aina yake.(Picha na Dewji Blog).

Baadhi ya Wanahabari walioshiriki kwenye Gala Dinner ya siku ya Uhuru wa Habari iliyoenda sambamba na Uzinduzi wa Mfuko wa Mwangosi kusaidia waandishi wa habari ambao wamepata matatizo wakiwa kazini.
Blogger Pamela Mollel (katikati) wa Jamii Blog ya jijini Arusha akibadilishana wanahabari wenzake Tonia Kasoni( kushoto) wa Radio 5 pamoja na Mhariri wa Sibuka TV wakati wa hafla hiyo.
Mjane wa Marehemu Daudi Mwangosi na mtoto wa mwisho wa marehemu wakati wa uzinduzi wa Mwangosi Fund utakaokuwa ukisaidia waandishi wa habari wanaopata majanga wakiwa kazini vile vile utaenda sambamba na Tuzo ya Mwandishi ambaye atakuwa amepata matatizo, misukosuko katika kutafuta habari za uchunguzi na Tuzo hiyo itakuwa ikitolewa kila mwaka Septemba 6 siku aliyokufa Daudi Mwangosi na mshindi wa Tuzo hizo atajinyakulia Milioni 10 zitakazotolewa na waendeshaji wa mfuko huu UTPC.
Mzee Kassim Mapili wa Mjomba Band akikung'uta gitaa wakati akipiga wimbo wa Mbaraka Mwishe" Njoo mjionee Morogoro"....wakati wa hafla ya kuchangisha fedha za mfuko wa Daudi Mwangosi zilizoenda sambamba na uzinduzi wa mfuko huo katika hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha.
Mmoja wa waandishi wa siku nyingi kwenye tasnia ya habari ambaye pia ni Mwanaharakati wa kutetea haki za Wanawake Bi. Leila Sheikh akiimba nyimbo za zamani pamoja na Mjomba Band inayoongozwa na Mzee Kassim Mapili na Mrisho Mpoto.
Bi. Leila Sheikh akisakata Rhumba la enzi hizo sambamba na Mzee Makwaiya Wakuhenga wakati Gala Dinner katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari Duniani kwenye Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa kuamkia leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Abubakar Karsan.
Wanahabari kutoka Zanzibar nao walijumika na wenzao wa Bara kutoka nchini za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Gala Dinner.

Wakongwe katika tasnia ya habari hapa nchini akiwemo Mzee Salim Salim na Mzee Hamza Kasongo na wenzao wakibadilishana mawazo.
Mgeni rasmi kwenye Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari duniani ulioenda sambamba na uzinduzi wa Kitabu kilichoandaliwa na Media Council Tanzania (MCT) pamoja na Kitabu cha Uhuru wa Vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Afrika Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akitoa salamu za Rais Kikwete za Pongezi kwa wanahabari Tanzania kwa kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari Duniani ambapo Serikali imeahidi kushirikiana na wanahabari bega kwa bega kwa mustakabali wa kuboresha tasnia hiyo.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akizindua Ripoti ya Habari hapa nchini ya mwaka 2012 iliyoandaliwa na Media Council of Tanzania (MCT) aliyeshika kitabu hicho ni Afisa Mipango Mwandamizi wa Taasisi ya Media Council of Tanzania (MCT) Bi. Alakok Mayombo na Mjumbe wa MCT Bw. Allan Lawa na MC wa Gala Dinner hiyo Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania Jane Mihanji.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene, Mwenyekiti wa Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera na mwakilishi wa Ubalozi wa Ireland kwa pamoja wakizuindua Kitabu cha Uhuru wa Vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Afrika kilichandaliwa na MISA katika Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akionyesha kitabu "SO THIS IS DEMOCRACY" mara baada ya kukizindua rasmi.

Usia Nkhoma wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na mwanahabari mwenzake wakifurahia jambo wakati wa hafla hiyo.

Mzee Hamza Kasongo akiendesha Harambee kwa wanahabari na wahariri kwa ajili ya kuchangisha mfuko wa Mwangosi utakaokuwa ukisaidia wanahabari pindi wapatapo matatizo kazini.
Stella Vuzo wa UNIC akitangaza ahadi yake binafsi ambapo ameahidi kutoa Dola 300 kuchangia Mfuko wa Mwangosi.
Mwenyekiti wa Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera akitoa ahadi yake binafsi ambapo ameahidi kuchangia Laki moja huku Misa-Tan imetoa ahadi ya Shilingi Milioni moja kuchangia mfuko wa Mwangosi uliozinduliwa rasmi usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha.
Mwakilishi kutoka BBC ambao nao pia waliguswa na kuchangia mfuko wa Mwangosi kiasi cha Shilingi Milioni Mbili.
Mwendeshaji wa Harambee hiyo Mzee Hamza Kasongo akitangaza kiasi cha fedha zilizokusanywa kwenye Harambee hiyo ambacho ni zaidi ya shilingi Milioni 19 wakati wa Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari duniani.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akikabidhi fedha taslim shilingi laki 5 zilizokusanywa kwenye Harambee hiyo kwa Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya.

TIGO BLOGGERS PARTY@NEW AFRICA HOTEL

$
0
0

Sports Lady pia niliwakilishaaaaaaaaaaaaaaaa

 Mmoja kati ya wageni waalikwa katika 'Party Mchapalo', iliyowakutanisha wadau wa Mtandano wa Simu za Mkononi Tigo na Wamiliki wa 'Magazeti Mtandao', (Blogers) akichagua kadi wakati ilipokuwa ikichezeshwa droo ya kuwapatia zawadi za Simu za mkononi, Ipad,na Moderm za tigo, mabloger hao, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya New Africa usiku wa jana(PICHA NA SUFIANI MAFOTO.COM)
 Baadhi ya wamiliki wa mitandao Pendwa, kutoka (kulia) ni mmiliki wa mtandao huu wa Sufianimafoto.com, Dina Ismail Blog, King Kiff Blog na Blogu ya wananchi, wakipozi kwa picha wakati wa hafla hiyo.
 
 Huku ndani wengine walikwishaanza kujisevia yaani 'kujidownlodia' vinywaji na kuapload vinywani mwao kama kawa, kama dawa.
 Kulia ni Meneja wa Mtandao huu Nasma Mafoto, akiwa na shosti wake waliyekutana  katika mchapalo huo.
 Na wanasa kumbukumbu nao hawakuwa nyuma katika kunasa kila tukio lililokuwa likijiri mahala hapo.
 Mwimbaji wa bendi ya Tanzanite, Frola Mkumbo, akiimba kuwaburudisha na kuwapagawisha mabloger, katika hafla hiyo. 
Kina dada nao walichuana kusebeneka na miondoko ya mduara kuwania Ipad na Simu ya mkononi.
Huyu ndiye aliyeibuka kidedea na kuondoka na Ipad...........
 
 Pande hizi wengine kila mmoja alikuwa akijitafuna tu......yaani 'akijiaplodi' vitafunwa.....
 Mr. Mulamula, naye alikuwepo pande hizo akitoa mawili matatu kuwahamasisha mabloger ili kusonga mbele.
 Mzee wa Daladala (kushoto) ndiye alikuwa akisherehesha mchapalo huo pande hizo, (kulia) ni Meneja Mauzo, William....akisubiri kukabidhi zawadi za washindi.
 Mr. William (kulia) akikabidhi zawadi ya Moderm kwa mmoja kati ya washindi wadroo iliyochezeshwa ukumbini hapo.
 Mzee wa Fullshangwe (kushoto) akipokea zawadi ya simu ya mkononi baada ya kujibu swali kwa ufasaha...
 Kajunason (kushoto) naye akipokea zawadi ya Ipad baada ya kuibuka kidedea kwa kuwashinda wenzake katika kusakata sebene na Black Dance...kama Mithun Chakalabot...
 'Snap' ya kumbukumbu.......na wadau wa mitandao.......

AZAM FC YAFA KIUME MOROCCO, YAPIGWA 2-1

$
0
0

Kipa wa AS FAr Rabat, Ali Grouni akimfariji mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco baada ya kukosa penalti ambayo ineipa Azam tiketi ya kufuzu Kombe la Shiriksiho jioni hii kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, Rabat. Azam imefungwa 2-1. 

Na Mahmoud Zubeiry, Rabat
SOKA ni mchezo wa bahati wakati mwingine. Naam sadakta, usemi huo umedhihirika leo kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah baada ya Azam kulala 2-1 mbele ya wenyeji AS FAR Rabat na kutolewa katika Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho Afrika, licha ya kupata nafasi nzuri ya kusonga mbele dakika ya 81.
“Tumekosa penalti dakika ya 81, siwezi kumlaumu refa ikiwa tumekosa penalti zimebaki dakika tisa,” alisema kocha wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall baada ya mchezo akizungumza na BIN ZUBEIRY.
Azam ilihitaji sare yoyote ya mabao ifuzu na ilikaribia kuipata dakika ya 81 ilipopata penalti ikiwa nyuma kwa mabao 2-1, lakini fundi wa upigaji wa michomo hiyo, John Raphael Bocco alikwenda kugongesha mwamba mpira huo.
Dakika ya 88, kona nzuri iliyochongwa na Khamis Mcha ‘Vialli’ iliunganishwa vizuri kwa kichwa na Bocco, lakini beki mmoja wa Rabat akaiwahi kwenye chaki na kuiondosha kwenye eneo la hatari.
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Abib Charef Medh aliyesaidiwa na Mahmoud Bitam na Mohamed Mekous wote kutoka Algeria, hadi mapumziko, Rabat walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Azam ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya sita, mfungaji John Raphael Bocco kwa mpira wa adhabu, baada ya beki mmoja wa Rabat kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Boko alipiga shuti zuri ambalo liliupita ukuta wa Rabat na kumpoteza maboya kipa wao, Ali Grouni na kutinga nyavuni.
Mashabiki wa Rabat walianzisha fujo baada ya bao hilo na kujikuta wakipambana na Polisi. Idadi ya Polisi iliongezwa uwanjani ili kuwadhibiti mashabiki hao ambao walikuwa wakivunja viti na kuwatupia Polisi.
Iliwachukua dakika sita tu Rabat kusawazisha kupitia kwa Abdelrahim Achchakir kwa mkwaju wa penalti, baada ya beki David Mwantika kumchezea rafu mchezaji wa Rabat.
Refa Abib Charef Medh alimtoa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja Achchakir kwa kumchezea rafu Brian Umony dakika ya 35.
Hata hivyo, Azam walishindwa kutumia mwanya wa Rabat kucheza pungufu na kujikuta wakifungwa wao bao la pili.
Mustafa Allaoui alipiga vizuri shuti la mpira wa adhabu umbali wa mita 25 na kumtungua Mwadini Ally dakika ya 42.
Baada ya bao hilo, wenyeji waliendelea kulisakama kama nyuki lango la Azam licha ya kucheza pungufu.
Viungo wa Azam walionekana kabisa kuzidiwa na viungo wa Rabat ambao waliifanya timu hiyo itawale mchezo. Azam haikufanya shambulizi la kushitua tangu wafungwe bao la pili.
Kipindi cha pili, mchezo ulizidi kuwa wa kasi na mashambulizi ya panede zote mbili, lakini kilianza vibaya kwa Azam, baada ya beki wake David Mwantika kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 56 kwa kumchezea rafu mchezaji wa Rabat.
Mwantika leo hakuwa katika ubora wake- kwani hata faulo alizocheza na kusababisha penalti ilikuwa ‘si ya lazima’ na hata kadi nyekundu pia angeweza kuiepuka kama asingemsukuma hadi kwenye lami mchezaji wa Rabat.  
Kutokana na Azam kubaki pungufu, Rabat walizidisha mashambulizi langoni mwa wageni na Kaddioui Yuossef alikuwa mwiba kwa timu ya Stewart.
Waziri Salum alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 75 baada ya kumchezea rafu Kaddioiu Yuossef.
Ajabu baada ya kadi hiyo, Azam walizinduka na kuanza kulishambulia kama nyuki lango la Rabat na ndipo dakika ya 81 beki mmoja wa Rabat alipounawa mpira kwenye eneo la hatari na refa akamuru penalti ambayo Bocco alikosa.
Wakati mashabiki wachache wa Tanzania waliokuwa uwanjani wakishangilia kwa kuamini Bocco anafunga, aligongesha mwamba mpira na kuinyima nafasi muhimu Azam.    
Baada ya mchezo huo, kocha Stewart alisema kwamba wamefungwa kwa sababu ya makosa ya safu ya ulinzi. “Kweli refa alikuwa wa upande mmoja, bao la pili (la Rabat) halikuwa sahihi, aliotea. Kadi ya Waziri haikuwa sahihi, walikuwa wanapambana (wachezaji), lakini bado siwezi kumlaumu ikiwa aliipa timu yangu penalti zimebaki dakika tisa,”alisema.
Azam sasa imetolewa kwa jumla ya mabao 2-1, baada ya awali wiki mbili zilizopita kutoka sare ya bila kufungana Dar es Salaam na Waarabu hao.
Rabat sasa watamenyana na moja ya timu zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa kusaka tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shikrikisho.
Katika mchezo huo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Kipre Tchetche, Salum Abubakar, John Bocco, Humprey Mieno/Gaudence Mwaikimba dk79  na Brian Umony/Khamis Mcha dk70.
AS FAR Rabat; Ali Grouni, Anouar Younes/Ennajar Tarik, Younes Hammal, Younes Belakhdar, Kaddoui Youssef, Abdelrahim Achchakir, Aqqal Salaheddine/Alloudi Soufiane, Mustafa Allaoui, El Kodry Yassine, El Bakkali Medamine na El Yousfi Mostafa.

DRFA YAZIPONGEZA RED COAST, ABAJALO & FRIENDS RANGERS

$
0
0

CHAMA cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimezipongeza timu zake tatu zilizofuzu kucheza Ligi ya Mabingwa, baada ya kumalizika kwa Ligi Daraja la Pili hatua ya sita bora Aprili 27 mwaka huu.  
Timu hizo ni Red Coast, Abajalo na Friends Rangers, zitakazoungana na timu za mikoa mingine kucheza Ligi ya Mabingwa itakayoanza Mei 12 mwaka huu chini ya Usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo, alisema ligi hiyo ilikuwa na ushindani wa hali ya juu na kuzitaka timu zilizofuzu hatua hiyo kujipanga vizuri ili kuuwakilisha vyema mkoa na hatimaye kucheza Ligi Daraja la Kwanza. 
“Kwa niaba ya DRFA napenda kuchukua nafasi hii kuzipongeza timu hizo kwa kufanya vizuri na kupata nafasi ya kuuwakilisha mkoa wa Dar es Salaam katika kutafuta kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao wa 2013/2014.
“Tunaamini watajiandaa vyema na kutuwakilisha vizuri katika ligi hiyo, kufanya kwao vizuri ndio itakuwa fahari yetu DRFA na wadau wa mpira wa miguu mkoa wa Dar es Salaam, tunawatakia kila la kheri na tupo pamoja katika kushirikiana nao.
Ligi Daraja la Pili hatua ya sita bora mkoa wa Dar es Salaam ilianza Aprili 15 mwaka huu ambapo ameziomba timu za Sharif Stars, Day Break na Boom FC zilizoshiriki ligi hiyo kujiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano yajayo.


OKWI, ULI, KIPRE, BOCCO, NIYONZIMA, SAMATA NA YONDAN WACHANUA TUZO ZA TASWA

$
0
0


Haji Manara, Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo 

KAMATI ya kusimamia Tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2012 zinazotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imepokea mapendekezo ya majina ya wanamichezo kutoka vyama mbalimbali kwa ajili ya kuwania tuzo hizo kwa kila mchezo.

Majina ya wanamichezo hao yamependekezwa na vyama husika, isipokuwa mpira wa miguu kwa wanaume pamoja na mpira wa kikapu, ambapo majina yameteuliwa na kamati kwa kushirikiana na baadhi ya wahariri wa habari za michezo na wadau wa michezo husika, ingawa awali vyama hivyo viliombwa kuwasilisha majina lakini havikutekeleza ombi hilo hivyo kamati ikaamua kutafuta utaratibu mwingine wa kupata majina.

Pia vyama viwili vya michezo ya  paralimpiki na baiskeli bado majina hayajaifikia kamati yetu kutokana na sababu mbalimbali na tayari wameahidi watawasilisha majina hayo kabla ya Mei 12 mwaka huu. Chama cha Mpira wa Wavu pia kimeshindwa kuwasilisha majina.

Hatua ya mwisho ambayo itafanyika baada ya kupokea mapendekezo hayo kwenye kila mchezo, Kamati ya Tuzo za Taswa itafanya uchambuzi kupitisha majina hayo kulingana na sifa ambazo vyama husika vimeleta kwa kila mwanamichezo na kuona kama wanastahili kupewa tuzo kulingana na vigezo vya kamati na TASWA.

Awali TASWA ilipanga tuzo hizo zifanyike Aprili 27 mwaka huu, lakini imeshindikana kutokana na sababu mbalimbali zilizokuwa nje ya uwezo wa Kamati ya Tuzo pamoja na chama kwa ujumla na sasa sherehe zitafanyika mwanzoni mwa mwezi Juni katika tarehe itakayotangazwa baada ya kukubaliana na wadhamini, ambapo mazungumzo yanatarajiwa kukamilika kabla ya Mei 15 mwaka huu.

Tunavishukuru vyama vyote vilivyotupa ushirikiano kwa hatua ya awali kwa kutupatia mapendekezo yao pamoja na kutaja sifa kwa kila mchezaji waliyewasilisha jina lake nasi tunaahidi tutapitia kwa umakini mapendekezo hayo, lakini uamuzi wa kamati ndiyo utakaokuwa wa mwisho.

TASWA itatoa tuzo kwa kila mchezo ambao kamati yetu ambayo  Katibu wake ndiye pia Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando itajiridhisha wanastahili, ambapo baadaye washindi wa kila mchezo watawania Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Tanzania kwa Mwaka 2012.Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Tanzania kwa mwaka 2011 ilienda kwa Shomari Kapombe. Washindi wengine kwa miaka ya karibuni ni Mwanaidi Hassan (2010 na 2009), Mary Naali (2008), Martin Sulle (2007) na Samson Ramadhan (2006).

Majina ya wanaowania kwa mwaka 2012:

MPIRA WA MAGONGO-WANAUME
Sylvester Kigodi
2.   Casto Mayuma
3.   Gurtej Bilu Singh
4.   Vendri Bhamra
5. Elias Samala

Gofu ya Kulipwa 
1 Hassani Kadio 
   2 Yassin Salehe
  3 Fadhili Nkya
  4 Salimu Mwanyenza
  5 Rajabu Iddy

GOFU YA RIDHAA WANAWAKE:

1:MADINA IDDI
2:ANGEL EATON
3. HAWA WANYECHE
4.AYNE MAGOMBE

GOFU YA RIDHAA WANAUME
Jimmy Mollel
Frank Roman
Nuru Mollel
Martin MacDonald
John Said


NGUMI ZA RIDHAA-WANAUME
  1. Ismail Isack Galiatano
  2. Said Hofu
  3. Selemani Kidunda.
  4. Victor Njaiti
  5. Mohamed Chibumbui.

NGUMI ZA RIDHAA WANAWAKE:-
1.   Sara Andrew
2.   Irene Kimaro
3.   Easter Kimbe.
4.   Mather George
5.   Mariam Nyerere.

Ngumi za Kulipwa
1.      Francis Miyeyusho
2.     Ramadhan Shauri
3.     Thomas Mashali
4.     Said Mbelwa
5.     Francis Cheka


JUDO-TANZANIA BARA-WANAUME

1)     AHMED MAGOGO
2)    ADREW THOMAS MLUGU
3)    GEOPHREY EDWARD MTAWA
4)    GERVAS LEONARD CHILIPWELI
5)    ABUU SELEMANI MCHETEKO
6)   ABUUBAKAR NZIGE

JUDO TANZANIA BARA WANAWAKE
                             
1.     MATRIDA .H. TEMBA
2.     AMINA MOHAMED

JUDO ZANZIBAR-WANAUME
1.    MOHAMMED KHAMIS JUMA
2.   MASOUD AMOUR KOMBO
3.   MBAROUK SULEIMANI SULEIMAN

JUDO ZANZIBAR-WANAWAKE
1.     GRACE ALPHONCE
2.     LAYLATI MOHAMMED

TENISI-WANAWAKE
 [1] Rehema Athumani
[2] Vailety Petar
 [3] Mkunde iddi
 [4] Edna John
 [5] Zuhura Baraka

TENISI  Wanaume
 [1] Omary Abdalah
 [2] Yassini Shabani
 [3] Hassan Kasimu
 [4] Kiango Kipingu
 [5] Lebric Jacobu

MPIRA WA MIKONO-WANAUME
Faraji Shaibu
Nyuki ZANZIBAR
Hemedi Salehe
JKT
Abinery  Kusena
JKT
Ally Khamis
Ngome
Hassani  Yusufu
Magereza

MPIRA WA MIKONO-WANAWAKE
Catherine    Mapua
Ngome
Dorisi        Mangara
Magereza
Zakia        Mohamed
Ngome
Happy      Mahinya
JKT
Mary       Kimiti
Magereza

RIADHA-WANAWAKE
1.Zakia Mrisho
2. Mary Naali
 3.Jacklin Sakilu
4.Sarah Ramadhani  
 5.Anjelin Tsere
6. Sara Maja

RIADHA-WANAUME
1. Dickson Marwa
 2. Faustine Musa
3. Augstino Sule
4. Bazil John
5. Samson Ramadhan

KRIKETI-WANAUME
1.   Abhik Patwa.
2.     Benson Mwita.
3.     Sefu Khalifa.
4.     Issa Kikasi.
5.   Riziki Kiseto
KRIKETI-WANAWAKE
Monica Pascal.
Mwanaiddi Ibrahim.
Hadija Nasibu
Esther Wales
Mwanaidi Ammy

SOKA-WANAWAKE
FATUMA MUSTAPHA
ASHA RASHID
MWANAHAMISI OMARY
SOPHIA MWASIKILI
ESTER CHABRUMA

SOKA-WANAUME
JOHN BOCCO-AZAM
KELVIN YONDANI-YANGA
SHOMARI KAPOMBE-SIMBA
MCHA KHAMISI-AZAM
MBWANA SAMATTA-TP MAZEMBE
Thomas Ulimwengu-TP Mazembe

WACHEZAJI WA NJE WANAOCHEZA TANZANIA
EMMANUEL OKWI-SIMBA(SASA ETOILE DU SAHEL)-SOKA
KIPRE TCHETCHE-AZAM-SOKA
HARUNA NIYONZIMA-YANGA-SOKA
HAMISI KIIZA-YANGA-SOKA
MARY WAYA-FILBERT BAYI –NETIBOLI (ALIKUWA KOCHA MCHEZAJI)

KIKAPU-WANAWAKE
Faraja Malaki- Jeshi
Evodia Kazinja-JKT Stars
            Sajida Ahmed-Don Bosco
           Rehema Kilomba-Donbosco
        Tukusubira David-Vijana Queens

KIKAPU-WANAUME
Mussa Chacha-Savio
Lusajo Samuel Mwakipunda-Oilers
Salim Mchemba-ABC
Filbert Mwaipungu-ABC
Steven Atanasio-ABC

NETIBOLI
Lilian Sylidion-Filbert Bayi
Mwanaidi Hassan-JKT
Irene Elias Kanile-Filbert Bayi
Jacqueline Sikozi-Filbert Bayi
Faraja Malaki-Jeshi Stars

WACHEZAJI BORA CHIPUKIZI

Salum Abubakari-Azam-soka
Frank Domayo-Yanga-soka
Edward Cristopher-Simba-soka
Emmanuel Malya-Tenisi Gymkhana Arusha
Tambwe Juma-Kriketi


WATANZANIA WANAOCHEZA NJE

Mbwana Samatta-TP Mazembe
Ivo Mapunda-Gor Mahia
Hasheem Thabeet-Oklahoma
Thomas Ulimwengu-TP Mazembe
Soud Abdulrazak-Uganda (kikapu)
Mohammed Abdallah ‘dulah’-Uganda (kikapu)

TUZO YA HESHIMA--- ITATANGAZWA UKUMBINI
TUZO YA MWANAMICHEZO BORA MWAKA 2012- ATAPATIKANA MIONGONI MWA WASHINDI WA KILA MCHEZO

Imetolewa na
Haji Manara
Mwenyekiti Kamati ya Tuzo TASWA
05/05/2013

RATIBA YA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA SASA KUPANGWA JUMANNE

$
0
0

Upangaji ratiba (draw) ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) uliokuwa ufanyike juzi (Mei 3 mwaka huu), sasa utafanyika Jumanne (Mei 7 mwaka huu) na ligi hiyo itaanza Mei 12 mwaka huu kama ilivyopangwa.

Uamuzi huo umefanya na Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana leo (Mei 5 mwaka huu) kujadili maandalizi ya ligi hiyo, yakiwemo maombi ya baadhi ya mikoa ambayo haijamaliza yao kutaka RCL isogezwe mbele.

Kamati ya Mashindano chini ya Uenyekiti wa Blassy Kiondo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ilipitia maombi hayo na kuangalia athari ambazo zinaweza kujitokeza huko mbele iwapo RCL itasogezwa mbele.

Baadhi ya athari iwapo RCL itasogezwa mbele ni timu zitakazopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutopata muda wa kufanya usajili wa wachezaji kwa msimu mpya.

Hivyo draw hiyo itakayofanyika saa 6 mchana itahusisha mikoa ambayo tayari imemaliza ligi na kuwasilisha majina ya mabingwa wao. Mabingwa ambao wamewasilishwa na mikoa yao kwenye mabano ni Abajalo SC (Dar es Salaam 2), Biharamulo FC (Kagera), Flamingo SC (Arusha), Friends Rangers (Dar es Salaam 3), Katavi Warriors (Katavi), Kiluvya United (Pwani), Kimondo FC (Mbeya) na Machava FC (Kilimanjaro).

Mingine ni Magic Pressure FC (Singida), Mbinga United (Ruvuma), Mji Njombe (Njombe), Polisi Jamii Bunda FC (Mara), Red Coast FC (Dar es Salaam 1), Rukwa United (Rukwa), Saigon FC (Kigoma), TECKFOLT FC ya Kilombero ambayo ni Shule ya Sekondari (Morogoro) na UDC FC ya Ukerewe (Mwanza).

Ada ya ushiriki ni sh. 100,000 wakati usajili wa wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika Ligi ya Mkoa na unatakiwa kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho. TFF inapenda kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya ligi hiyo.

Mikoa iliyoshindwa kuwasilisha mabingwa wake ni Dodoma, Geita, Iringa, Lindi, Manyara, Mtwara, Shinyanga, Simiyu, Tabora na Tanga.

AZAM FC KUREJEA NYUMBANI KESHO MCHANA

$
0
0

Timu ya Azam inatarajiwa kurejea nchini kesho (Mei 6 mwaka huu) saa 7 mchana kwa ndege ya Emirates kutoka Morocco ambapo jana (Mei 5 mwaka huu) ilicheza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya AS FAR Rabat ya huko. 
Azam ilipoteza mechi hiyo kwa mabao 2-1, hivyo kutolewa katika raundi ya pili ya mashindano hayo. Mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam timu hizo zilitoka suluhu.

STARS KUANZA NA SHELISHELI MICHUANO YA COSAFA

$
0
0

Taifa Stars imepangwa kundi A la michuano ya Kombe la COSAFA ambapo itacheza mechi yake ya kwanza Julai 6 mwaka huu jijini Lusaka, Zambia dhidi ya Shelisheli.

Upangaji ratiba (draw) wa mashindano hayo ulifanyika juzi (Mei 3 mwaka huu) jijini Lusaka ambapo timu nyingine zilizo na Taifa Stars katika kundi hilo ni Namibia na Mauritius. Kundi la Taifa Stars litachezea mechi zake jijini Lusaka.

Mechi ya pili ya Taifa Stars katika hatua ya makundi itakuwa Julai 8 mwaka huu dhidi ya Mauritius. Mechi ya mwisho katika hatua hiyo itakuwa Julai 10 mwaka huu dhidi ya Namibia.

Kundi B lina timu za Kenya (Harambee Stars), Botswana (Zebras), Lesotho na Swaziland. Hatua itakayofuata baada ya hapo ni ya mtoano (knockout) na kila kundi litatoa timu moja tu.

Iwapo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itafuzu kwa hatua itakayofuata itacheza Julai 13 mwaka huu na Afrika Kusini (Bafana Bafana) ambayo pamoja na timu nyingine tano zimekwenda moja kwa moja katika hatua ya mtoano.

Nyingine zilizokwenda moja kwa moja hatua ya mtoano ni wenyeji Zambia, Angola, Zimbabwe, Msumbiji na Malawi ambazo kwenye viwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ziko juu ya zile zilizoanzia hatua ya makundi.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, fainali ya michuano ya Kombe la COSAFA itafanyika Julai 20 mwaka huu.

SIMBA YACHUMPA NAFASI YA TATU YA VPL

$
0
0
WEKUNDU wa Msimbazi Simba Sc wamejikusanyia pointi tatu jioni ya leo baada ya kuwabanjua maafande wa Ruvu Shooting kwa mabao 3-1, katika mchezo wa ligi kuu Bara uliopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini dar es Salaam.
Ushindi huo umeifanya Simba ifikishe pointi 42 na hivyo kupanda kutoka nafasi ya nne hadi ya tatu ya msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Yanga ambao tayari wameshatwaa ubingwa wakiwa na pointi 57, huku Azam Fc ikiwa ya pili kwa pointi 48.
Katika mchezo wa leo Simba pamoja na ushindi huo Simba watajilaumu sana baada ya nyota wake kukoisa mabao mengi ya wazi.
Alikuwa Amri Kiemba aliyeanza kuifungia Simba bao la kwanza katika dakika ya 14, bao ambalo lilibadilisha hali ya mchezo na timu kuanza kushambuliana.
Hata hivyo timu hizo zilikwenda mapumziko kwa Simba kuongoza kwa bao 1-0.
kipindi cha pili kilianza kwa taratibu ambapo mabadiliko kwa kila timu yaliweza kuingeza ushindani huku wachezaji wakichezeana rafu za hapa na pale.
Mwamuzi wa mchezo aliwazawadia kadi za njano kwa sababu tofauti,Mrisho Ngassa wa Simba, Said Madega na Ernest ernest wa Ruvu Shooting.
Katika mchezo huo anmbao Simba ilipambwa na wachezaji chipukizi zaidi, Edward Christopher aliiandikia bao la pili kabla ya Ismail Mkoko kuandika la tatu dakika mbili baadaye. 
Katika mchezo wa leo, Simba iliwatoa Haruna Chanongo, Felix Sunzu na Ramadhan Singano na kuwaingiza Ismail Mkoko, Mrisho Ngassa na Edward Christopher, huku Shooting iliwatoa Said Dilunga, Said madega na Rafael Kagalu na kuwaingiza Kulwa Mfaume, Hamis Kisuke na Ayoub Kitale.

HATIMAYE CLOUDS MEDIA WAMFUNGUKIA LADY JAYDEE

$
0
0
RUGE MUTAHABA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
UONGOZI wa Clouds Media Group kwa kupitia Mkurugenzi wao wa Utafiti na Matukio, Ruge Mutahaba, umemtaka msanii wa Bongo Fleva, Judith Wambura, Lady Jay Dee ajipange na kupokea changamoto badala ya kutafuta mahali kwa kujiegemeza kwa kueneza matusi kwao.
Clouds Media leo wamefungua  mdomo kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miezi mitano tangu Jay Dee alipokuwa akiwarushia makombora kwa madai kuwa wameharibu soko la muziki wa Bongo Fleva sambamba na kuitangaza bendi ya Skylight kwa ajili ya kuiangamiza Machozi Bendi.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam ambapo pia alikuwa akirushwa moja kwa moja katika redio ya Clouds FM, Mutahaba alisema Jay Dee amekuwa akilalamikia mambo mawili ambayo ni bendi ya Skylight na matangazo yake yaliyoshindwa kurushwa hewani japo alilipia Sh 240,000.
Alisema suala hilo walilimaliza baada ya kumueleza kuwa redio yao haiwezi kukataa matangazo kwakuwa ndiyo wanayowafanya waendelee kuwa kinara katika suala zima la kuiendesha Clouds FM.
“Nilimwambia kamwe hatuwezi kukataa matangazo na kama kuna lolote limefanyika, basi ni kwa bahati mbaya, ukizingatia kuwa tayari alishafanya kazi nyingi pamoja na kupewa urahisi kwenye kazi zake kwa kupitia Clouds FM.
“Pamoja na yote hayo, bado matusi na kejeli yaliendelea hasa katika mitandao ya kijamii jambo lililotufanya tuamuwe sasa kujibu japo hapo kabla tuliamua kubaki kimya kwa ajili ya kulinda hadhi ya kazi zetu,” alisema.
Kuhusu shutuma za kuitangaza zaidi Skylight Bendi, Ruge alisema bendi hiyo si mali ya Joseph Kusaga, Mkurugenzi wao wala yeye, kama madai hayo yanavyotolewa bila kufanya utafiti, isipokuwa ni mali ya Sebastian Ndege.
“Kama kuna mvutano kati ya Machozi Bendi na Skylight basi ni wa kibiashara maana wote wanalipa fedha za matangazo na kama chanzo ni Jay Dee kuporwa wanamuziki wake, hilo si jambo geni kwenye muziki.
“Dada yangu Asha Baraka asingekuwa makini angelia sana, maana kila bendi inayoanzishwa au kuendeshwa lazima ichukuwe wanamuziki kutoka kwake, ukizingatia kuwa ni jambo la kawaida hivyo tumuomba Jay Dee atumie busara katika hili pamoja na kuumiza kichwa kupokea ushindani na changamoto kama hizo za kuchukuliwa wanamuziki,” aliongeza Ruge.
Aidha, Ruge alisema Clouds FM ni redio ya watu binafsi, hivyo si ina utaratibu wake katika utendaji wa kazi, ikiwapo kuchagua nyimbo au kuacha kupiga kama kuna mtu amekwenda kinyume, hasa wale wanaopita nje na kuanza kuwatusi, kuwakejeli bila kukumbuka fadhira walizofanyiwa kabla ya kuwa maarufu wao.
Pia alisema Clouds FM ipo tayari kufanya majadiliano ya wazi na mtu yoyote mwenye hisia tofauti juu yao, huku ikiwataka wasanii waongeze bidii katika kazi zao ili wasimlaumu mtu wanapoanguka na kuwapisha wengine, maana muziki unaonekana ni wa kupokezana vijiti.
Katika siku za hivi karibuni katika vyombo vya habari hasa hasa kwenye mitandao ya kijamii nchini kumekuwa na taarifa rasmi na zisizo rasmi kutoka kwa Mwanamuziki Lady Jaydee alilalamikia Kituo chetu cha Clouds FM na wakurugenzi wake Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga.

TAARIFA KAMLI YA RUGE HII HAPA

Kwa mtazamo wangu, kila mwananchi ana haki ya kutoa maoni yake ingawa kwenye nchi yetu ya Tanzania, tumezoea maoni hayo kutolewa kwa lugha ya ustaraabu na staha. 
Maoni kuhusu nani wa kuja kwenye msiba wako au nyimbo za kupigwa kwenye msiba wako ni haki ya kila mwananchi na hakuna atayeuingilia uamuzi huo. Maoni pia ya redio gani mtu anaipenda au tv gani pia nayo ni utashi wa mtu mwenyewe. 
Uongozi wa Clouds FM ulikuwa umefikia maamuzi ya kutojadili jambo hili kutokana na kuamini kuwa ni tatizo binafsi la mtu na sio jambo lenye maslahi ya Taifa hivyo kwa uhalali linahitaji majadiliano au mazungumzo binafsi. 
Sura ambayo jambo hili limewekwa na kulifanya kama dharura ya kitaifa sio sahihi kabisa kutokana na kukosekana na hoja za kina za kuhitaji majibu na pili kukosekana kwa ujumla wa tija kwa tatizo hili kitaifa. 
Bado ninaamini linatakiwa kubaki kama tatizo la mtu binafsi ila inapofika taarifa zikapotoshwa kwa nia ya kuwapa mtazamo tofauti wasikilizaji wetu, Clouds FM inataka kuweka maslahi ya wasikilizaji, wabia wetu wa biashara na watanzania wote mbele kwa kuwapa taarifa sahihi za jambo hili. 
Clouds Media Group inapata lawama kubwa sana kutoka kwa watu wengi ambao pamoja na kuunga mkono ukimya wetu wanajiuliza ni kwanini hatukufanya jitihada za kumaliza tatizo hili bila kufika hatua iliyofikia sasa ya matusi, kebehi na vitisho kutwa vinavyoelekezwa kwetu na pia vinaendelea kuichafua tasnia ya muziki hasa hasa Bongo flava; ambayo imefika mahali inaonekana kila changamoto inayomkabili msanii wa Bongo flava lazima itatuliwe kwa njia za mabavu (matusi, vitisho na kuchafuana). 
Lawama hizo sio za kweli na naomba nirudi nyuma kidogo kwenye historia ya jambo hili. Tarehe 14 mwezi wa 12 mwaka 2012 kwenye tweeter account ya Jaydee, alipost kifuatacho:  
Nilichofanya ni kumpigia simu na kuzungumza nae.  Akasema sijaandika kwenye blog chochote, nikamwambia Jide mi nakuheshimu sana. Nimekupigia kwasababu naamini kama kuna kitu chochote ni bora nisikie kwako, nategemea na wewe pia utanipigia iwapo kuna jambo lolote lile.  Tulikotoka sisi hatutakiwi kuendeshwa na majungu na maneno ya mtaani.Hiyo ilikuwa tarehe 14 mwezi December mwaka jana. Baada ya kama dk 10 hivi akanitumia msg ( ambazo bahati nzuri nilizihifadhi) na kusema ni kweli alikuwa ananizungumzia mimi kwa sababu kuna vitu kadhaa vinamsumbua na aliambiwa mimi ndo nilihusika navyo. 
La kwanza, ‘nililipa matangazo ya shs laki mbili na 40 ila hayajachezwa na wala sijarudishiwa hela yangu, nimeambiwa umekataza matangazo yangu ya Nyumbani lounge yasipigwe’.  
La pili, naruhusu watangazaji wangu wamtukane ikiwa ni pamoja na kupromote zaidi bendi ya Skylight. 
Pamoja na kwamba yeye alinitumia message, mimi nilimpigia simu na kumpa ufafanuzi wa yote hayo niliyosema hapo juu. 
Nikasema, Biashara yetu sisi ni matangazo…..kwanini tukataze matangazo yako yasipigwe?? Labda bahati mbaya tu, jamaa anayebook matangazo alipitiwa kuyabook kibinadamu ila Gadna si anakuja hapa kila wakati, kwann asimkumbushe tu?? Tutayasogeza tu mbele hadi wiki inayofuata, kwanini niyakataze wakati muda sio mrefu tumetoka kuleta biashara ya Repa bora wa bendi hapo hapo Nyumbani lounge. 
Niliendelea kujibu kuwa sio kweli kabisa, siwezi kuruhusu jambo kama hilo na kama ni kweli mtangazaji anamtukana anifahamishe ni nani na kwenye kipindi gani, nitasikiliza kipindi na kama ni kweli nitamfukuza kazi ( Clouds ina mitambo ya kuhifadhi matangazo yake yote kwa takribani miezi 9).
Hili nilimjibu kwa kirefu kidogo ikiwemo kumwambia akaze buti maana Skylight Band wanakuja juu nk nk. (Skylight Band ni bendi inayofanya vizuri sana hapa mjini na ilipoanza ilichukua baadhi ya majina makubwa kutoka Machozi Band). 
Baada ya kumaliza mazungumzo tuliagana vizuri tu kwa miadi ya kukutana nikirudi maana nilikuwa safarini. 
Kwahiyo ukiniuliza Jaydee anacholalamika ni nini??? Jibu langu litakuwa ni hayo mambo mawili maana hata nyie watanzania wenzangu mnaosoma mitandao ya kijamii mtakubaliana na mimi kuwa amekuwa anashambulia personality zetu, mimi na Mkurugenzi mwenzangu bila kuweka wazi hoja za msingi kuhusu yale anayotutuhumu nayo.  Nimejitahidi sana kuelewa tatizo lake hasa ni nini na imekuwa inanipa shida kidogo?? Nimejitahidi sana kufikiria ni mirija ipi ya biashara kwake imeingiliwa, nakosa majibu???  
Clouds FM ni ya watu na watu wanaweza kufanya makosa kweli na hata kusababisha matangazo ya laki 2 na 40 yasirushwe, kwa hilo nilishazungumza na Jaydee na kuomba radhi toka tarehe 14 December 2012. Clouds FM haina ubia wowote ule na Skylight Band (ni bendi iliyoanzishwa na Mtanzania)hivyo kuipromote ni katika misingi ile ile ya biashara kama tunavyopromote bendi yeyote ile na vilevile Clouds FM pia haihusiki kabisa na kutetereka kwa biashara ya chakula, vinywaji na bendi inayofanyika Nyumbani lounge. Inashangaza hata kuhusishwa na biashara ya Nyumbani lounge…!!! 
Sina ugomvi binafsi na Jaydee wala Gadna, na tarehe 12 February mwaka huu, nilienda kuazima stools kwa ajili ya shooting kutoka kwenye sehemu yao ya biashara ingawa yeye amekiri kuwa na ugomvi mkubwa na sisi binafsi na Clouds kama chombo. 
Nyimbo yake iliyotoka ya Joto Hasira ilipokelewa vizuri sana kulinganisha na nyimbo mbili zilizopita ‘Yeye’ na ‘Mimi ni mimi’ ambazo hazikufanya vizuri pamoja na jitihada kubwa ya kuzipromote. Joto Hasira iliacha kupigwa kutokana na shinikizo lake mwenyewe, ikiwa imeshachezwa mara 48 ndani ya wiki tatu toka imetoka wote tulipigwa na bumbuwazi na kujiuliza ni kitu gani tumefanya kuambiwa hatupigi nyimbo na lawama nyingine. Kama ofisi tukaona tukae kimya na kusubiri hatua inayofuata ukizingatia tuliendea kupiga nyimbo na video hata baada ya maneno makali ya mwanzo. Kauli haikubadilika, mbaya zaidi kauli za kebehi na kuchafuana zikaongezeka hadi kufikia uamuzi wa sisi kama taasisi kuamua rasmi kutopiga nyimbo zake hadi atakapofuta kauli zake na kuomba msamaha. 
Kupiga au kutopiga nyimbo kwa kituo cha redio ni jambo la kawaida na kwasababu ni chombo binafsi ni muhimu kwa watu kama Jaydee na wasanii wengine (na hata wananchi wa kawaida) kuelewa kuwa kila ofisi ina taratibu zake na iwapo utatokea ukiukaji wa taratibu hizo, policy ndo zinaongoza maamuzi.  Hebu tujiulize, mbona sio mjadala wa Taifa msanii Diamond hapigwi karibu miezi sita sasa kwenye station ya Magic FM, Ray C na Ali Kiba kwa karibu mwaka mzima walikuwa nyimbo zao na video hazipigwi na East Africa hadi walipoomba msamaha, hadi Yanga kwa muda mrefu walikuwa hawatangazwi habari zao kwenye chombo kimoja cha habari. Hayo ni mambo ya ofisi binafsi na hakuna anayeweza kulaumu maamuzi hayo. 
‘Management reserves the right of admission’……nani hajaona kibao hiki kwenye hoteli nyingi tu nchini, nani asiyefahamu kuwa kuna hoteli ambazo ukienda kama mwanamke peke yako unakataliwa? Hizi ni taratibu na kila mahali zipo…..hata nyumbani lounge ndo maana Sam Machozi ambaye yuko Skylight Band zamani alikuwa mwanamuziki wa Machozi Band amepigwa marufuku pale Nyumbani lounge na halalamiki maana ni sehemu binafsi na ina taratibu zake. Ni tofauti na sehemu za wazi za umma kama Mnazi mmoja au kituo cha basi cha Magomeni.
 Clouds Media Group inafuata taratibu zote za nchi na za kimkoa ila na yenyewe pia inaweka taratibu zake za uendeshaji. Sasa isifike mahali Clouds inapoweka taratibu zake hizo na kuzitekeleza inaonekana inafanya makosa.  Yaani hata tarehe za kufanya show nchi hii tunatakiwa kupeleka maombi sehemu ili watu zaidi ya mmoja wasifanye show kweli??? Kwanini tunachanganya ushindani na fitina…..acha ziwepo bendi 10 zinazoshindana, kuanzishwa kwa bendi nyingine kusiangaliwe kama fitna.  Na hata mtu akianzisha bendi kwa kuchukua wanamuziki kutoka kwenye bendi nyingine, si ndio dhana ya ushindani??? 
Kama ni kulalamika kuanzishwa kwa bendi nyingine au kuchukuliwa wanamuziki, Dadaangu Asha Baraka si angeshafanya maandamano nchi nzima. Ila wote tunatambua kuwa ni jasiri ndo maana anatulia na kuanza upya. 
Mbona watu hawalalamiki  baa zinapofunguliwa 10 mtaa mmoja, au saloon za nywele, moja jirani na nyingine. Ni lazima tukubali na tuzoea ushindani. 
Pamoja na ushindani kingine ninachoomba  kuwasihi watanzania wenzangu hasa hasa wasanii wetu  zaidi ni kuwa kila mtu na kila kitu kina ‘shelf life’. Watu wa zamani naamini wanamkumbuka Power Mabula….alikuwa anatisha sana wakati ule. Au nani anaweza kusahau umaarufu wa Mzee Nobert Chenga na Kundi la Muungano cultural troupe au labda huko ni nyuma sana; nani anamkumbuka Kanda Bongo Man, alicharge laki moja enzi hizooo….au labda hapa katikati umaarufu wa Muumini, Mr Nice au mtu kama Saida Karoli (alijaza Stadium). Wote hao walikuwa maarufu sana. Sasa wasanii hawa na wengine wanaokuja wasipojiandaa kuelewa kuwa kila kitu kina muda wake, tutakuwa na taifa la vijana ambao asubuhi mpaka jioni badala ya kuhangaikia fursa nyingi zilizopo wataishia kutafuta mtu wa kumlaumu. 
Ni lazima Edibily Lunyamila atarithiwa sehemu yake na kina Mrisho Ngassa ambaye naye muda utapita ni lazima atawaachia kina Simon Msuva. Wapo watu kama kina Dully Sykes walioanza kujiandaa kwa kuwaachia kina Diamond na wao kufungua studio na kuwa maproducer. Suala la kupokezana vijiti halikwepeki kuanzia makazini, mpirani na hata kwenye sanaa. Cha kufanya ni kujiandaa kwa maisha yako baada ya kugawa kijiti chako. 
Taarifa za kutaka kuua muziki wa Bongo flava kwa makusudi zinashangaza, ili iweje sasa??? Clouds inategemea matangazo ya biashara kama asilimia 95 ya mrija wa mapato na muziki tunaopiga redioni ni sehemu ya maudhui kwahiyo hakuna namna yeyote ile tutataka muziki huo upotee. Tunafanya juhudi zote hizi kwasababu tunahitaji nyimbo bora na wasanii bora ili tuweze kuendelea kuwa kituo bora cha redio.
SUMMARY YA MSIMAMO WETU
Fursa: 
Uganda endorsment
TZ ringtones
Album sales – Kina Mamu.
DVD live performance shows.
Meeting ya wasanii wote watoe maoni.




IBF YAMPONGEZA CHEKA KWA KUONESHA KIWANGO CHA JUU KWENYE MASUMBWI

$
0
0

MONDAY 06, MAY, 2013 – DAR ES SALAAM, TANZANIA - Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) limempongeza bondia maarufu wa kitanzania Francis Cheka (pichani)kwa juhudi zake za kuwa bondia mzuri mwenye viwango vya kimataifa katika uzito wa Super Middleweight.
Francis Cheka aliweza kutetea mkanda wake wa IBF Africa uzito wa Super Middle baada ya kumshinda kwa KO bondia Thomas Mashali aka “Simba asiyefugika” tarehe 1 Mei, 2013 katika ukumbi wa PTA jijini Dar Es Salaam. 
IBF inachukua fursa ya kumpongeza Francis Cheka baada ya ushindi huo ambao umedhihirisha kuwa yeye kweli ni bingwa wa bara la Afrika. Francis Cheka atarudiana na bondia wa Malawi Chimwemwe Chiotcha mwezi wa Agusti katika mpambano la kutetea mkanda wake.
Mpambano wao wa marudiano utafanyika katika jiji la Blantyre nchini Malawi na tayari majadiliano ya mpambano huo yanaendelea vizuri. Kampuni ya “Mawenzi Boxing Promotion” ya nchini Malawi chini ya bwana Stephen Mawezni ndiyoitakayoandaa mpambano huo.
Pambano hili linakuja baada ya wadau kadhaa wa ngumi kuomba mabondia hao warudiane walipoonyesha ujuzi mkubwa na ushindani katika mpambano wao Desemba 26 mwaka jana katika uwanja wa Sheikh Amri Abeidi jijini Arusha siku ya Boxing Day.
Baada ya mpambano huo, IBF itampatia Francis Cheka nafasi ya kugombea mkanda wa IBF wa Kimataifa (IBF International Super Middleweight) na mabondia wa Ulaya au Marekani. Hii ni kudhihirisha kuwa Francis Cheka hana tena mpinzanai nchini Tanzania na kumpambanisha na mabondia wa kitanzania ni kumpotezea muda na uwezekano wake wa kutengeneza jina na pesa.
Wakati huo huo bondia Thomas Mashali bado ni bingwa wa Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBF) katika uzito wa Middle kwani mkanda wake haukuwa kati ya mikanda iliyogombewa kwenye mpambano uliomalizika Mei mosi.

NDOLANGA APONGEZA FIFA KUSIMAMISHA UCHAGUZI TFF, AISHAURI TFF KUTORUDIA MAKOSA

$
0
0

RAIS wa Heshima wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alhaj Muhidin Ndolanga amelipongeza Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa kubatilisha mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa TFF na kuagiza zoezi kufanyika upya.
Fifa ilifikia uamuzi huo kufuatia kuwepo  baada ya kubaini kasoro iliyotokana na ukosefu wa kutokuwepo vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadili.
FIFA ambayo ilituma ujumbe wake katikati ya mwezi uliopita kufanya utafiti kuhusu mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF ambao ulisimamishwa baada ya baadhi ya wagombea kulalamika, imetaka uchaguzi ufanyike kabla ya tarehe 30 Oktoba 2013, lakini ukitanguliwa na mabadiliko ya katiba ambayo yatahusisha uundwaji wa vyombo vya kushughulikia ukiukwaji wa maadkwa utata wa zoezi hilo uliotokana na kuenguliwa kwa baadhi ya wagombea bila ya sababu za msingi, huku pia mchakato huo ukiendeshwa kwa katiba batili.
Akizungumza kwenye kipindi cha Spoti leo kinachorushwa na Redio One juzi, Ndolanga alisema hadhani TFF kama itavurunda tena zoezi hilo kama ilivyokuwa awali.
Ndolanga ambaye alikuwa ni mmoja ya wadau waliohojiwa na Fifa juu ya utata wa uchaguzi huo alisema kwamba, anaamini TFF itajipanga vizuri katika hilo ili haki iweze kutendeka kwa kila mmoja.
“Sidhani kama hivi sasa tutaendeleza matatizo ya awali, Katiba ilivunjwa na kubadilishwa kwa waraka hivyo naamini itarekebishwa kwa mujibu wa taratibu na kisha tuendelee na taratibu nyingine.
Aidha, Ndolanga alitoa rai kwa wajumbe wa mkutano mkuu kuwa makini katika zoezi la kubadilishwa kwa katiba ya TFF  kwa kuhakikisha wanaingiza vitu ambavyo vitaleta faida kwa Taifa zima la Tanzania.

YANGA LAZIMA WAKASHEREHEKEE UBINGWA CHUMBANI-JULIO

$
0
0


KOCHA msaidizi wa timu ysa soka ya Simkbas, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amejinasibu timu yake kutibua furahas ya ubingwa wa mahasimu wao Yanga, katika mchezo wao wa ligi kuu bara utakasopigwa Mei 18 kwenye Uwanjua wa Taifa.
Yanga tayari  imetwaa ubingwa huo ulikuwa ukishikiliwa na Simba  kabla ya kumalizika kwa ligi hiyo.
Alisema kikosi cha kipo imara kwa mechi hiyo na hivyo Yanga itarajie kipigo nkitakatifu siku hiyo ambacho kitavuruga shamrashara zao za kusherehekea ubingwa wa ligi hiyo.
“Tutahakikisha tunakimwagia mchanga kitumbua cha Yanga hivyo waende kusherehekea ubingwa wao wakiwa wamejifungia ndani kwa aibu ya kipigo,”alisema
Julio aliongeza kuwa kwa sasa kikosi chake kinaendelea na mazoezi ya kawaida ya mechi zake zilizosalia kwenye ligi hiyo ambapo kabla ya kuivaa Yanga, keshokutwa wataikaribisha Mgambo Shooting, mechi itakayopigwa kwenye uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam.
Simba ambayo jana iliibamiza Ruvu Shooting kwa mabao 3-1 kwa sasa imefikisha pointi 42 ambazo zimeiwezesha kupanda hadi nafasi ya tatu ya ligi hiyo kutoka ya nne.
Katika mechi yao ya mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

TWO HOT DALTONICS CHARITY CONCERTY

Viewing all 454 articles
Browse latest View live