Quantcast
Channel: Sports Lady
Viewing all 454 articles
Browse latest View live

RED COAST, KARIAKOO, SAIGONI KUANZIA NYUMBANI RCL

$
0
0

Upangaji ratiba (draw) ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) umefanyika leo (Mei 7 mwaka huu) huku mabingwa wa mikoa ya Dar es Salaam (Red Coast), Lindi (Kariakoo) na Kigoma (Saigoni) wakianzia nyumbani katika ligi hiyo itakayoanza Mei 11 au 12 mwaka huu.

Ligi hiyo itachezwa kwa mtoano kwa mtindo wa nyumbani na ugenini ambapo mwenyeji atapanga tarehe ya mechi ambazo zinatakiwa kuchezwa kati ya Jumamosi au Jumapili. Mechi za marudiano katika raundi hiyo ya kwanza zitachezwa kati ya Mei 18 na 19 mwaka huu.

Katika upangaji huo ulioshuhudiwa na waandishi wa habari kwa niaba ya klabu husika, mabingwa wa Mkoa wa Shinyanga (Stand Ngaya FC) wamepita moja kwa moja hadi raundi ya pili itakayochezwa kati ya Mei 25 na 25 mwaka huu wakati mechi za marudiano ni kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu.

Raundi ya tatu itachezwa kati ya Juni 8 na 9 mwaka huu wakati marudiano ni Juni 15 au 16 mwaka huu. Raundi ya nne itachezwa kati ya Juni 22 au 23 mwaka huu wakati marudiano ni Juni 29 au 30 mwaka huu. Raundi ya tano ni kati ya Julai 6 na 7 mwaka huu na marudiano ni Julai 13 au 14 mwaka huu.

Timu tatu ndizo zitakazopanda kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao, ambazo ni ya kwanza nay a pili wakati timu ya tatu itapatikana kwa timu zilizoshindwa hatua ya nusu fainali kucheza zenyewe kwa zenyewe. Washindi wa nusu fainali nao watacheza wenyewe kwa wenyewe ili kupata bingwa wa RCL ambaye atakabidhiwa kombe la ubingwa.

Ligi hiyo inashirikisha mabingwa kutoka mikoa 27 ya kimpira ambapo katika raundi ya kwanza wanaanza mabingwa 26, raundi ya pili ni mabingwa 14 wakijumuisha na bingwa wa Shinyanga ambaye katika draw ameingia moja kwa moja katika hatua hiyo.

Raundi ya tatu itashirikisha timu saba zilizosonga mbele pamoja na moja yenye uwiano mzuri wa matokeo ili kufanya jumla ya timu nane. Raundi ya nne itakuwa na timu nne. Wakati raundi ya tano itakuwa ni kumpata bingwa na mshindi wa tatu.

Katika upangaji huo wa ratiba mechi za raundi ya kwanza (timu ya kwanza ikianzia nyumbani) itakuwa kama ifuatavyo; Red Coast vs Abajalo, Kariakoo vs Mtwara, Friends Rangers vs Kiluvya United,  TECKFOLT FC vs African Sports, Machava FC vs Flamingo SC, Gunners United vs Manyara na Simiyu vs Magic Pressure FC.

Nyingine ni Polisi Jamii Bunda FC vs UDC FC, Geita vs Biharamulo SC, Saigoni SC vs Tabora, Katavi Warriors vs Rukwa United, Mji Njombe vs Mbinga United na Kimondo FC vs Iringa.

Mechi zitachezwa katika viwanja vya makao makuu ya mikoa, vinginevyo kuwepo na maombi rasmi ambayo yatakubaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).



AFISA UTAMADUNI MKOA WA TANGA ATEMBELEA KAMBI YA MISS UTALII ILIYOPO MKOANI HUMO

$
0
0

Afisa Utamaduni Jiji la Tanga, Peter Semfuko (katikati) ,Matron Hilda Mwinyi (Kulia), na Mratibu wa kamati ya maandalizi Kessy Salum Mbasha (Kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2013, alipo kwenda kukagua kambi na kuzungumza na warembo hao Jana katika hoteli ya Mwambani Tanga Beach.

Wakati Maandalizi ya fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2013 yanaendelea kwa kasi katika hoteli ya kitalii ya Mwambani iliyopo katika ufukwe wa Tanga, huku kila Mrembo akijifua vikali, Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Tanga Ndugu Peter Semfukwe ametembelea kambini hapo, kujionea yeye mwenyewe warembo wa Miss Utalii Tanzania 2013 ambao wanajiandaa na Fainali hizo za Taifa zitakazo fanyika wiki Ijayo,kasha alizungumza nao na kuwakaribisha mkoani Tanga.
Afisa Utamaduni  alisema  kuwa amefurahi kukutana na warembo wote wakiwa katika Afya Njema, Mvuto na kila mmoja kuonekana ndiye atakaye twaa taji hilo la Miss Utalii Tanzania 2013, pia ameipongeza kamati ya maandalizi kwa juhudi na jitihada kubwa za kuandaa mashindano hayo ambayo dhima yake ni kuutangaza utalii wa ndani pamoja na utamaduni wa Mtanzania.  Aliongeza kuwa anaahidi  ushirikiano mkubwa wa hali na mali wakati wa maandalizi mpaka mwisho wa mashindano hayo.
Akizungumza na Warembo wa Miss Utalii Tanzania 2013 pamoja na Kamati ya Maandalizi ya Miss Utalii Tanzania , Afisa Utamaduni aliwaasa warembo hao wawe na heshima, adabu, na pia wawe ni mfano bora wa kuigwa katika jamii ikiwa ni warembo hao kuwa mstari wa mbele katika kushiriki, kutangaza Utalii na Utamaduni wa Mtanzania.
Mpaka sasa Kambi ya Miss Utalii Tanzania 2013 ipo jijini Tanga Mwambani Hotel na inaendelea Vizuri, Warembo zaidi ya 30 kutoka mikoa yote nchini ,wanajiandaa vizuri  kwa ajili ya Fainali Hizo zitakazo fanyika wiki ijayo Tanga, Kanda Maalum ya Zanzibar na Vyuo vikuu Tanzania.
Akizungumzia, juu ya maendeleo ya kambi, Fredy Njeje, alisema kuwa baada ya kukwamishwa na wadhamini walio toa ahadi hewa, wamelazimika kuhamishia shindano hilo mkoani Tanga,baada ya kuvutiwa na mwamko wa wafanya biashara na makampuni ya Jiji la Tanga wa kuwa na uwezo wa kudhamini matukio makubwa ya kitaifa na kimataifa.
Tunakabiliwa na changamoto ya warembo wengi kuwa wapya katika kambi yetu,baada ya wale waliokuwako kambini kabla ya kambi kuahirishwa kushindwa kurudi kambini kwa sababu mbalimbali,zikiwemo za kimasomo na wengine kukata tama baada ya kuahirisha. Hata hivyo tayali nafsi zao zimechukuliwa na washindi wa pili wa mikoa yote ambayo warembo wake wameshindwa kurudi kambini, na tayali warembo 30 wameripoti kambini na tunategemea wengine 10 kuripoti kambini wakati wowote ili kufikisha idadi ya warembo 40 wata kao panda jukwaani. Tumejiandaa na tunapata ushirikiano mkubwa kwa serikali ya mkoa nay a Jiji la Tanga, hivyo kutuhakikishia kuwa tarehe itakayo pangwa sasa haitabadilika tena wala kuahirishwa. Tarehe kamili ya shindano itatangazwa kesho na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ambaye pia ni Afisa Utamaduni wa Jiji la Tanga.
Washindi wa 1-5 wa Fainali za Taifa ,watawakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya Dunia na nchi yatakako fanyika katika mabano  International Miss Tourism World (Marekani), Miss Tourism United Nation (Mexico), Miss Heritage World (Tunasubiri Taarifa), Miss Tourism University World(Tanzania), Miss Globe International (Uturuki), Miss Tourism World ( Equatorial Guinea ), Miss Freedom Of The World ( Kosovo) , na Miss Tourism United Nation (Nigeria)  n.k

Wakati huohuo, katika kuhakikisha kuwa maandalizi ya Fainali za taifa, za mashindano hayo ambapo mkoa wa Tanga unakuwa wenyeji kwa mara ya kwanza yanafanyika kwa ubora na hayakwami, kamati ya maandalizi ya kimkoa umeundwa ambayo mwenyekiti wake ni Peter Semfuko Afisa Utamaduni wa Jiji la Tanga. Miss Utalii Tanzania ,hadi sasa tunashikilia Jumla ya mataji 5 ya Dunia na kimataifa, yakiwemo ya Miss Tourism World 2005-Africa,Miss Tourism World 2006-SADC,Miss Tourism World 2007-Africa, Miss Tourism
Model Of The World 2008-Personality, Miss Africa 2006 – 1ST Runner Up n.k

Asante,
 Fredy Njeje
Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano ya Umma


BONDIA SAID MBELWA AMGALAGAZA SAID MKONDE KWA K,O

$
0
0

Bondia Omari Zungu akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Haruna Sinondo wakati wa mchezo wao uliofanyika Chanika mwishoni mwa wiki iliyopita Sinondo alishinda kwa K,O raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Said Mkonde kushoto akioneshana uwezo wa kurushiana makonde na Said Mbelwa wakati wa mpambano wao uliofanyika Chanika mwishoni mwa wiki iliyopita Mbelwa alishinda kwa K,o raundi ya pili.


Bondia Said Mkonde kushoto akioneshana uwezo wa kurushiana makonde na Said Mbelwa wakati wa mpambano wao uliofanyika Chanika mwishoni mwa wiki iliyopita Mbelwa alishinda kwa K,o raundi ya pili.
Bondia Chilambo Hemed kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Boniface Urasa wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki Chanika Chilambo alishinda kwa point. 

Bondia Said Mbelwa akipambana
Bondia Omari Zungu akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Haruna Sinondo wakati wa mchezo wao uliofanyika Chanika mwishoni mwa wiki iliyopita Sinondo alishinda kwa K,O raundi ya pili. 
Refarii Saidi Chaku akimwinua mkono juu Bondia saidi Mbelwa kuashilia ni mshindi katika mpambano huo.


-

SIMBA, MGAMBO SHOOTING HAPATOSHI UWANJA WA TAIFA KESHO

$
0
0

Timu za Simba na Mgambo Shooting ya Tanga zinaumana kesho (Mei 8 mwaka huu) katika mchezo pekee wa Ligi Kuu ya Vodacom utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza saa 10.30 jioni vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa VIP C na B wakati VIP A ni sh. 20,000.

...MECHI YAO NA RUVU SHOOTING  YAINGIZA MIL 17
Mechi namba 111 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Ruvu Shooting na Simba iliyochezwa juzi (Mei 5 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kushinda mabao 3-1 imeingiza sh. 17,700,000.

Watazamaji 3,163 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 3,485,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 2,700,000.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 2,901 na kuingiza sh. 14,505,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 28 na kuingiza sh. 560,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 1,772,416.50, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 1,063,449.90, Kamati ya Ligi sh. 1,063,449.90, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 531,724.95, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 206,781.93 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 206,781.93.

SIMBA YATAKATA MWANA WAKE...YANGA WAJIPANGE

$
0
0
Mfungaji wa bao la Simba, Haroun Chanongo, wa pili kutoka kushoto akishangilia na Ramadhani Singano 'Messi'. Kulia ni wachezaji wenzake wakimpongeza. 


Na Mahmoud Zubeiry, MEI 8, 2013
SIMBA SC imefufua matumaini ya kucheza michuano ya Afrika mwakani, kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Mgambo jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Andrew Shamba, aliyesaidiwa na Abdallah Rashid na Abdallah Mkomwa wote kutoka Pwani, hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na kiungo hatari wa pembeni, Haroun Athumani Chanongo dakika ya nane, ambaye aliombea mpira katikati ya Uwanja na kuanza kuwapangua mabeki wa Mgambo kabla ya kumchambua kipa Godson Mmasa.
Baada ya bao hilo, Simba SC waliongeza kasi ya mashambulizi langoni mwa Mgambo na Amri Kiemba alikaribia kufunga mara mbili wakati Nassor Masoud ‘Chollo’ na Ramadhani Singano ‘Messi’ kila mmoja alikaribia kufunga mara moja.
Kipindi cha pili, Mgambo JKT walipambana kutoruhusu mabao zaidi, ingawa Simba SC iliendelea kutawala mchezo huo kwa pasi maridadi na soka ya kuvutia.
Katika mchezo huo, kipa Juma Kaseja aliokoa hatari mbili tu kipindi cha kwanza moja alipopangua shuti la juu kabla ya kudaka na kipindi cha pili alipodaka shuti la chini, pembeni.
Ushindi huo, unaifanya Simba SC itimize pointi 45, sasa ikizidiwa tatu na Azam FC inayoshika nafasi ya pili, ambayo Jumapili itamenyana na Mgambo kwenye Uwanja wake wa Azam Complex, Chamazi.  
Katika mchezo wa leo, kocha Mfaransa Patrick Liewig aliwapumzisha wachezaji kadhaa tegemeo, Mrisho Ngassa, Shomary Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu na Mussa Mudde kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga Mei 18.   
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’/Omary Salum, Haruna Shamte, Miraj Adam, Hassan Khatib, Jonas Mkude, Edward Christopher, William Lucian ‘Gallas’/Rashid Ismail, Amri Kiemba, Ramadhani Singano ‘Messi’/Salim Kinje na Haroun Chanongo.
JKT Mgambo; Godson Mmasa, Salum Mlima, Ramadhani Kambwili, Bashiru Chanacha, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Chande Magoja/Mussa Gunda, Peter Mwalyanzi, Issa Kandulu, Fully Maganga na Nassor Gumbo. 

TATU BORA LIGI KUU YA VODACOM:  
                   PWDLGFGAGDPts
1Yanga SC 25176245143157
2Azam FC 24146442202248
3Simba SC25129438231545

MISS KIGAMBONI KUSAKWA JUNI 7@NAVY BEACH

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
SHINDANO la kumtafuta mrembo wa kitongoji cha Kigamboni mwaka huu "Redd's Miss Kigamboni 2013" linatarajiwa kufanyika Ijumaa Juni 8 kwenye ukumbi wa Navy Beach kuanzia saa 2:00 usiku hapa jijini Dar es Salaam.
Tayari warembo wameshaanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na shindano hilo ambapo wanajifua kwenye ukumbi wa Break Point (VIP) uliopo Posta hapa jijini.
Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yako katika hatua za mwisho na bado wanakaribisha warembo wenye sifa za kushiriki shindano hilo kufika mazoezini kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini.
Mratibu huyo alisema kwamba lengo la kuweka wazi na kuwahamasisha warembo ni kutaka kutoa nafasi kwa wasichana wengi zaidi kujiandikisha na hatimaye kupata mshindi atakayekiwakilisha vyema kitongoji hicho katika mashindano ya ngazi ya Kanda yatakayofanyika baadaye mwezi ujao.
"Tumeshaanza maandalizi na tunawaomba wadau wa sanaa ya urembo wa hapa nchini kujiandaa kusubiri Kigamboni kutoa mrembo wa taifa mwaka huu, tunawashiriki wenye mvuto na sifa za ushindani," alisema Somoe.
Aliongeza kwamba fomu kwa ajili ya kushiriki shindano hilo zinapatikana bure na warembo wanafanya mazoezi chini ya Blessing Ngowi, ambaye mwaka juzi alishiriki fainali za taifa za Redd's Miss Tanzania na alitwaa taji la Kanda ya Elimu ya Juu.
Alisema pia makampuni na taasisi mbalimbali zinakaribishwa kudhamini shindano hilo ambalo mwaka jana lilitoa mshindi katika kinyang'anyiro cha Kanda ya Temeke ambaye ni Edda Sylivester.
Edda alifanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye fainali za taifa huku mshindi wa taifa ni Brigitte Alfred ambaye mwaka huu ataenda kupeperusha bendera ya nchi katika mashindano ya dunia.

MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI TFF KUFANYIKA SEPTEMBA 29

$
0
0

Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unatarajiwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu baada ya ule wa Dharura wa marekebisho ya Katiba ulipangwa kufanyika Julai 13 mwaka huu.

Tarehe hizo zimepangwa na kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya TFF kilichofanyika leo (Mei 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa Rais wake Leodegar Tenga ambacho kupokea rasmi maagizo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na kupanga utekelezaji wake.

“Kamati ya Utendaji ya TFF imepokea rasmi barua ya FIFA na kupanga utekelezaji wake. Tumepokea maagizo ya FIFA yanayotuelekeza cha kufanya, si TFF wala mtu mwingine yeyote anayeweza kuongeza jambo lingine.

“Maagizo ni undeni Kamati ya Maadili, Kamati ya Rufani ya Maadili, fanyeni marekebisho ya Katiba, anzeni tena uchaguzi, waliokuwepo na wengine wapya waruhusiwe. Tumejitahidi kuhakikisha uchaguzi uwe kabla ya Oktoba 30 mwaka huu kama FIFA walivyotuagiza,” amesema Rais Tenga wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kazi kubwa itakuwa ni kutayarisha kanuni hizo, kwani Kamati za Maadili lazima ziwe na kanuni zake na kuhakikisha kuwa hakuna mgongano kati ya Kanuni za Nidhamu na Kanuni za Maadili.

Pia Rais Tenga amesema kuna kazi ya kuangalia jinsi zitakavyoingia katika uchaguzi ambapo maana yake muda wa mchakato wa uchaguzi utakuwa zaidi ya siku 40 za sasa, hivyo mabadiliko hayo yatagusa vilevile Kanuni za Uchaguzi.

Kwa mujibu wa ratiba ya utekelezaji, rasmu ya mwanzo ya Kanuni hizo inatakiwa iwe imetoka kufikia Mei 30 mwaka huu ambapo itapelekwa FIFA kwa ajili ya kupata mawazo yao kabla ya kuendelea na hatua inayofuata.

Juni 15 mwaka huu Kamati ya Utendaji ya TFF itakutana kupokea mapendekezo hayo ambapo baada ya kuyapitisha itayapeleka tena FIFA. Taarifa (notice) ya Mkutano Mkuu wa Dharura ambayo kikatiba ni siku 30 itatolewa Juni 12 au 13 mwaka huu.

Baada ya Mkutano Mkuu wa Dharura wa marekebisho ya Katiba, Kamati ya Utendaji itakutana kati ya Julai 14 na 15 mwaka huu kuunda Kamati ya Maadili na Kamati ya Rufani ya Maadili ili kuruhusu mchakato wa uchaguzi uanze.

MHASIBU MKUU JAMBO LEO AFARIKI DUNIA

$
0
0
Aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, marehemu Vick Mgoyo.
MHASIBU Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts (T) Limited inayochapisha gazeti la Jambo Leo, Staa Spoti, Dar Metro na jarida la Jambo Brand Tanzania, Vicky Mgoyo (49), amefariki dunia.
Meneja Mkuu wa Jambo Concepts, Ramadhani Kibanike, alisema marehemu Vicky Mgoyo alifariki dunia leo asubuhi kwenye Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam alikokimbimbizwa kupatiwa matibabu baada ya kuzidiwa usiku wa kuamkia leo.
Alisema kifo cha Vicky zaidi akijulikana kwa jina la Mama Mgoyo kimeacha pengo kubwa si tu kwa familia yake bali pia kwa Kampuni ya Jambo Concepts kutokana na kwamba alikuwa ni mtu mwaminifu kazini, lakini pia uhusiano mzuri na wafanyakazi wenzake.
"Tumepoteza mfanyakazi ambaye ni mchapa kazi na kipenzi cha wengi, tutamkumbuka kwa hilo. Naomba wafanyakazi tuungane na ndugu na jamaa katika kuomboleza msiba wa kipenzi chetu huku tukiamini kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.
"Bado hatujapata taarifa rasmi za maziko, ila taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda mkoani Kilimanjaro nyumbani kwao zinaendelea kufanyika," alibainisha Kibanike.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Juma Pinto alitoa mwito kwa wafanyakazi kuonesha mshikamano katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi kwa kuondokewa na mfanyakazi mwenzao.
Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, Anicetus Mwesa, akizungumzia msiba huo alisema Mama Mgoyo ametwaliwa na Mungu ilhali akiwa bado anahitajika na familia pamoja na ofisi yake, hivyo ameacha pengo ambalo litachukua muda kuliziba.
"Mwenzetu ametangulia nasi tupo nyuma yake, zaidi tumwombee ili Mungu ampumzishe katika raha ya milele," alisema Mwesa.
Kwa upande wake Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hili, Richard Mwaikenda, alisema atamkumbuka Vicky kwa kuwa ni mwanamke shupavu ambaye alikuwa anazingatia maadili ya kazi yake ya uhasibu.
Pia alisema alikuwa ni mama mjane makini ambaye alihakikisha anasimamia watoto wake katika suala la kuwapa elimu bora, ambapo katika hilo alikuwa akifanya kila anachoweza kuhakikisha anasomesha nje ya nchi tena kwenye shule bora na makini.
Vicky Mgoyo aliyezaliwa Novemba 26, 1964, ameacha watoto watatu huku wawili kati yao ni wanaume.
Alilazwa katika Hospitali ya Kairuki wiki iliyopita ambako alipatiwa matibabu kwa muda wa siku nne na kuruhusiwa.Jumatatu aliripoti kazini na kuendelea na kazi hadi jana jioni, ambapo usiku alizidiwa na hatimaye leo asubuhi Mungu alimchukua. Mungu ailaze pema peponi roho ya Vicky Mgoyo.

KOCHA MKUU TP MAZEMBE ABWAGA MANYANGA

$
0
0

KOCHA mkuu wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidem,okrasia ya Congo (DRC) Lamine Ndiaye ametangaza kujiuuzulu wadhifa wake huo.
Taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa jana imeeleza kwamba kocha huyo ameamua kuachia ngazi baada ya klabu hiyo kutupwa nje kwenye michuano ya CAF.
Rais wa klabu hiyuo Moses Katumbi,alitangaza uamuzi wa kocha huyo kujitoa kuifundisha klabu hiyo na kusema kuwa hawana budi kukubaliana na uamuzi huo.
Hata hivyo, Rais huyo amezuiia kuondoka kwa kocha huyo na kumpatia kazi nyingine ndani ya klabu hiyo.

MOYES ARITHI MIKOBA YA FERGUSON MAN U

$
0
0

Uongozi wa Old Trafford umetangaza rasmi na kuthibitisha kuwa David Moyes (pichani) atakuwa meneja mpya wa timu hiyo kuchukua nafasi ya Sir Alex Ferguson atakayestaafu mwishoni mwa msimu huu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Old Trafford mchana wa leo, David Moyes amepewa mkataba wa miaka sita wa kuifundisha Manchester United kuanzia msimu ujao.
Taarifa zaidi zinafuata.
BBC SWAHILI

HARDMAD ANAOMBA SUPPORT YAKO KILI MUSIC

$
0
0

Wimbo wa "tunda" ni wimbo ambao umefanya vizuri sana kule jamaica hata kupelekea baadhi ya wasanii wa kule kuifanyia upya instrumental yake yaani kufanya riddim...Ni msani anayestahili tuzo ya reggae ya killi mwaka huu

HOMA YA PAMBANO LA WATANI:YANGA WABAKI DAR, SIMBA WAENDA ZENJI

$
0
0
HOMA ya pambano la watani wa jadi nchini Simba na Yanga imezidi kupanda ambapo sasa timu hizo zimeamua kuingia kambini kwa ajili ya hukiandaa na mechi hiyo ya ligi kuu bara itakayopigwa Mei 18 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Ni kawaida kwa timu hizo zinapokjaribia kukwaana kuingia mafichoni, lakini Yanga ambayo tayari imeshatwaa ubingwa wa ligi hiyo imedai haina mpango wa kwenda mafichoni na kesho Ijumaa wachezaji wake wataingia kambini kwenye hosteli za klabu hiyo zilizopo mtaa wa jangwani.
Ofisa habari wa Yanga, Baraka Kizuguto amesema leo kwamba mechi yao ya Simba ni ya kawaida sana hivyo hawana sababu ya kwenda kujichimbia mahali na kuongeza kuwa kikosi kipo kamili na lazima waibuke na ushindi siku hiyo.
Kwa upande wa Simba ambayo imevuliwa ubingwa, kikosi chake kitaondoka kesho kwenda Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.
Simba inayonolewa na Mfaransa Patrick Liewig kupitia kwa kocha wake msaidizi Jamhuri Kihwelo 'Julio' imeweka wazi kwamba siku hiyo ni lazima wakimwagie mchanga kitumbua cha Yanga ili kutibua furaha zao za ubingwa.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

DRFA YAZIWEZESHA ABAJALO, RED COAST & FRIENDS RANGERS

$
0
0


Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almas Kassongo (kushoto), akimkabidhi  Mwenyekiti wa Red Coast,  Jumanne Ayubu Sh 700, 000 ikiwa ni mchango wa chama hicho kusaidia timu hiyo katika Ligi ya Mabingwa inayotarajiwa kuanza Mei 12 mwaka huu



CHAMA Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimezizawadia timu zake tatu za Red Coast, Abajalo na Friends Rangers zilizofanikiwa kucheza Ligi ya Mabingwa inayotarajiwa kuanza Mei 12 mwaka huu.

Makabidhiano hayo yalifanyika jana Alhmaisi (Mei 9) jioni kwenye ofisi za chama hicho, zilizopo makutano ya mtaa wa Mafia na Bonde, ambapo Red Coast waliokuwa washindi wa kwanza walikabidhiwa Sh 700, 000, huku Abajalo wao wakizawadiwa Sh 600, 000 na Friends Rangers wakijipatia Sh 500, 000.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo, lengo la timu hizo kukabidhiwa fedha hizo Viongozi waliohudhuria makabidhiano hayo kutoka DRFA ni Mkurugenzi wa Ufundi, Joseph Kanakamfumo, Afisa Tawala, Said Pambalelo,  Mjumbe wa Kamati ya Ufundi na Mashindano, Daudi Kanuti na Mweka Hazina Ally Hassani.

Wawakilishi wa timu ni Mwenyekiti wa Red Coast, Jumanne Ayubu, Meneja wa Friends Rangers, Shaaban Marsila na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Abajalo, Abbasi Ngau.

Wakati huo huo, kamati ya ufundi ya DRFA kesho Jumamosi Harbours Club Kurasini, itakutana na Viongozi wa soka la Wanawake (TWFA), Viongozi wa soka la Vijana na Kamati ya Waamuzi ili kupanga utaratibu wa ligi na pia kuandaa kozi ya makocha.




KAGERA SUGAR, RUVU SHOOTING KUUMANA KAITABA KESHO

$
0
0

Kagera Sugar inaikaribisha Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo pekee wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) utakaofanyika kesho (Mei 11 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kaitba mjini Bukoba.

Ingawa timu zote mbili hazipambani kutafuta ubingwa ambao tayari umetwaliwa na Yanga wala kukwepa kushuka daraja, mechi hiyo bado ni muhimu kwao katika mazingira matatu tofauti.

Kagera Sugar inayonolewa na kocha mkongwe kuliko wote katika VPL, Abdallah Kibaden na ikiwa na pointi 40 yenyewe inasaka moja kati ya nafasi nne za juu ambazo zina zawadi kutoka mdhamini wa ligi, lakini pia timu zinazoshika nafasi hizo za juu zinapata tiketi ya kucheza michuano ya BancABC Super 8.

Kwa upande wa Ruvu Shooting ya Kocha Charles Boniface Mkwasa yenye pointi 31 inasaka moja ya nafasi sita za juu ambazo ni fursa ya kuingia kwenye Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) ambayo inatarajiwa kuundwa baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Septemba 28 mwaka huu.

Wagombea nafasi za uenyekiti na makamu wake ni lazima watoke katika timu zilizoshika nafasi sita la juu katika VPL msimu uliopita. Uchaguzi wa TPL Board utafanyika siku moja kabla ya ule wa TFF uliopangwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu.

Raundi ya 25 ya ligi hiyo itakamilika keshokutwa (Mei 12 mwaka huu) kwa mechi kati ya wenyeji Azam na Mgambo Shooting ya Tanga. Mechi hiyo namba 169 itachezwa katika Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Azam yenye pointi 48 inahitaji moja zaidi ili kutetea nafasi yake ya umakamu bingwa iliyoutwaa msimu wa 2011/2013 na kupata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Wakati Azam ikisaka pointi hiyo moja, Mgambo Shooting inayofundishwa na wachezaji wa zamani wa mabingwa wa Tanzania Bara mwaka 1988, Mohamed Kampira akisaidiwa na Joseph Lazaro ni moja ya timu ziko katika hatari ya kurudi Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao.

Mgambo Shooting inahitaji pointi moja tu katika mechi mbili ilizobakiza kukwepa kurudi FDL, ikishindwa kupata pointi hiyo huku Polisi Morogoro na Toto Africans ya Mwanza zikishinda mechi zao za mwisho kwa uwiano mzuri wa mabao itakuwa imekwenda na maji.

Mechi ya Azam dhidi ya Mgambo Shooting itachezeshwa na refa Jacob Adongo kutoka Mara, na atasaidiwa na Abdallah Rashid wa Pwani na Charles Mbilinyi wa Mwanza. Mwamuzi wa mezani atakuwa Idd Lila wa Dar es Salaam wakati Kamishna ni Omari Walii wa Arusha.

SIMBA, MGAMBO SHOOTING WAINGIZA MIL.16

$
0
0

Mechi namba 149 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Mgambo Shooting iliyochezwa juzi (Mei 8 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kushinda bao 1-0 imeingiza sh. 16,651,000.

Watazamaji 3,006 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 3,226,125 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 2,539,983.05.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 1,640,402.54, tiketi sh. 3,175,000, gharama za mechi sh. 984,241.53, Kamati ya Ligi sh. 984,241.53, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 492,120.76 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 382,760.60.


KARIBU UBURUDIKE NA MALEGENDARY WENZAKO NDANI YA JOLLY'S CLUB KILA J'MOSI NA DJ JD

$
0
0
Unakumbuka? raha za ki-Legendary za muziki wa Silent Inn, Bills, FM Club, Carlifonia Dreamers, Mambo Club na Tazara? Basi DJ John Dillinga (DJ JD) na DJ Fast Eddy tunawakaribisha kujumuika na malegends wenzenu kila Jumamosi kuenzi nyakati hizo Isumba Lounge, Jolly Club kwa mchango wa elfu 10 tu mlangoni, Karibuni Sana.

KWA NINI SERIKALI IINGILIE MIGOGORO YA BAADHI YA WASANII ?_CHEMUNDUGWAO

$
0
0

Chemundugwao kushoto akiwa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Viajana na Michezo, Amos Makalla.

MIMI NASHANGAA SANA JUU YA SERIKALI PALE BIFU ZINPOKEA KWA RUGE BASI UINGILIA KATI KUTAFUTA SULUHU KWA KWELI KUNAACHA MASWALI MENGI.
KWA MTAZAMO WA KIUNGWANA NI  JAMBO JEMA SANA WALAKINI YANGU KWANINI IWE KWA RUGE TU AWALI WAZIRI NCHIMBI AKIWA NAIBU WA WIZARA YETU YA HABARI UTAMADUNI,VIJANA NA MICHEZO  AMEINGILIA KATI JAMBO LA RUGE NA MBILINYI (SUGU) NA SASA TUNASIKIA RUGE NA LADY J DEE SERIKALI IMEINGILIA KATI.
KUMBUKA ASHA BARAKA WA TWANGA PEPETA NA MAMAA WA MASHUJAA HATA  TAFF NA BONGO BOVIE, VIKUNDI VYA TAARABU NI BAADHI TU LAKINI WENGI WAPO WALIKUWA KWENYE MVUTANO MKALI LAKINI SERIKALI IKIWA KIMYA
USHAURI WANGU HATUA HIYO NZURI SANA KULETA AMANI KWA WASANII LAKINI IWE KWA WOTE BILA KUBAGUA WATATUE INAPOTOKEA MIGOGORO HATA YA KIMASLAHI PIA KUONDOA DHANA KUWA RUGE ANAPENDELEWA SERIKALI MADHARA YAKE KWA HISIA HIZO NI KUBWA SANA,KUSIPO ZIBA UFA KUTAJENGA UKUTA TUCHUKUE HATUA SASA, MAANA SISI NDIO TUPO KARIBU NA WASANII MUDA MWINGI TUNAWAMBUSHA SERIKALI JUU YA UMUHIMU WATOA HUDUMA SAWA KWA WOTE BILA KUJALI UMAARUFU WA MSANII KWA KUANZISHA DAWATI LA  HUDUMA KWA WASANII ITASAIDIA SANA

MIMI
CHE MUNDUGWAO
MWENYEKITI- CHAMA CHA MUZKI ASILI TANZANIA NA
MJUMBE WA BODI SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA
MKURUGENZI WA USHIRIKIANO- SHIRIKISHO LA MU

BARAZA LA WAZEE YANGA LAMHADHARISHA MWAMUZI WA MECHI YA WATANI

$
0
0

Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga mzee Ibrahim Akilamli (katikati) akiongea na wandishi wa habari makao makuu ya klabu leo
Kuelekea mchezo dhidi ya Simba SC mei 18, Baraza wa wazee wa klabu ya Young Africans limeomba mwamuzi wa mchezo huo achezeshe kwa kufuata sheria 17 zote za mchezo na kwa kufanya hivyo mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom watoto wa Jangwani lazima wataibuka na ushindi katika mchezo huo.
Akiongea na wandishi wa habari kwa niaba ya baraza la wazee makao makuu ya klabu, katibu mkuu wa baraza la wazee Mzee Ibrahim Akilimali (Ibrahimovich) amesema wanaamini kikosi cha Yangaa kitaibuka na ushindi katika mchezo huo ikiwa mwamuzi atachezesha kwa kufuata sheria zote 17 na kanuni za soka.
Akilimali amesema Yanga ni timu bora kwa sasa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kila mmoja anajua hilo, tuna wachezaji wazuri wenye kiwango cha hali ya juu ambao wamepikwa wakapikika wakaiva matunda ya mafunzo yao ndio yaliyotupatia ubingwa kabla ya ligi kumalizika.
Aidha aliongeza kuwa "Tunaahidi kwamba tutamfunga Simba SC siku ya mei 18 kutokana na umoja wetu, mshikamano na uongozi bora chini ya mwenyekiti Yusuf Manji na makamu wake Clement Sanga ambao mpaka sasa wameifnaya timu ya Yanga kuwa ya kuogopewa ukanda wote huuu".
Naye Mzee Hashim Mwika aliongeza kuwa waanahidi ushindi katika mchezo huo, idadi ya mabao haijalishi lakini kikubwa tunasema lazima tumfunge Simba mei 18 kikubwa tunaomba mwamuzi achezeshe kwa kufuata kanuni 17, na kama wakifanya hivyo basi Simba Sc wajiandae kupokea mvua ya mawe siku hiyo.
"Mwaka jana walitufunga kwa sababu hatukuwa pamoja, hatukua na maelewano lakini hivi sasa Yanga ni moja kuanzia viongozi, wachezaji, makocha na wanachama hivyo tunamini kwa kuwa pamoja na timu yetu bora lazima simba achezee kichapo "alisema mzee Mwika.
chanzo:www.youngafricans.co.tz

BREAKING NEWS; YANGA WATUA PEMBA KUWEKA KAMBI YA KULIPA 5-0 MEI 18 TAIFA

$
0
0
Yanga SC

Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA MEI 10, 2013 SAA 10:45

KIKOSI cha Yanga SC kimewasili kisiwani Pemba saa moja iliyopita kuweka kambi ya kujiandaa na mpambano dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC Mei 18, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga wameondoka kwa siri kubwa leo Dar es Salaam kwa ndege maalum ya kukodi, kwenda visiwani humo kujiandaa na pambano hilo la marudiano la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
BIN ZUBEIRY inafahamu Yanga imefikia katika hoteli ya Samail Morden, mkabala na benki ya PBZ na kesho itaanza mazoezi kwenye Uwanja wa Gombani.
Yanga itakuwa huko hadi siku moja kabla ya mechi itakaporejea Dar es Salaam na kufikia katika hoteli moja kubwa Jijini, kabla ya kuamkia kwenye mechi siku inayofuata.
Pamoja na kwamba Yanga tayari imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu, lakini inaipa uzito mkubwa mechi hiyo kwa sababu inataka kulipa kisasi cha kufungwa 5-0 na wapinzani wao hao wa jadi mwaka jana.
Tangu umeingia madarakani, uongozi wa Yanga chini ya Mwenyekiti, Alhaj Yussuf Mehboob Manji umekuwa ukiumia kichwa na kipigo cha 5-0 mwaka jana.
Mara kadhaa Manji amewahi kukaririwa na BIN ZUBEIRY akisema kwamba 5-0 zinamuumiza kichwa hasa katika wakati ambao idadi ya mabao katika mechi za timu hiyo ilipungua.
Wakati Yanga wametua Pemba, kuna wasiwasi Simba SC ikaachana na utamaduni wake wa kuweka kambi Zanzibar kujiandaa na mechi dhidi ya wapinzani wao hao.
Kihistoria, Simba SC imewahi kuipa Yanga vipigo viwili vitakatifu 6-0 mwaka 1977 na 5-0 mwaka jana, wakati Yanga iliifunga SImba 5-0 mwaka 1969.  
Safari hii, Yanga imepanga kuweka heshima kwa kuhakikisha inaipa kipigo kitakatifu Simba cha kuvunja rekodi ya 6-0.

YANGA KULAMBA MIL.70 KUTOKA VODACOM

$
0
0

Meneja Uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim (Katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wakati kampuni hiyo ilipotangaza Zawadi kwa washindi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2012/13. Kampuni hiyo imetangaza kutumia zaidi ya Tsh Milioni 200 kwa ajili ya zawadi kwa washindi wa ligi kwa ujumla. Pamoja  nae ni Meneja Uhusiano wa  Umma wa Vodacom ,Matina Nkurlu (Kushoto) na Afisa habari wa TFF. Boniface Wambura.


Mdhamini  wa Ligi Kuu ya soka Tanzana Bara, Kampuni ya Vodacom imetangaza kutumia kiasi cha Shilingi Mil 200 kwa ajili ya kutoa zawadi ya fedha taslimu katika ligi inayomalizika mei 18 ambapo sasa Machampioni wa msimu huu watajinyakulia Shilingi Milioni 70.
Mbali ya bingwa, Vodacom pia itatoa fedha kwa timu inayomaliza nafasi ya pili, ya tatu na  ya nne katika msimamo wa ligi ambazo ni Sh. 35 Milioni,  huku Sh. 25 Milioni na Sh. 20 Milioni zote zikiwa na ongezeko ikilinganishwa na zawadi za fedha zilizotolewa katika msimu wa 2012 / 2013.
Zawadi hizo zimetangazwa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kampuni hiyo kupitia Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim, ikiwa ni pamoja na kuainisha zawadi za washindi wa mchezaji mmoja mmoja pamoja na timu iliyoonyesha nidhamu kwa msimu huu.
"Mwaka huu tutatumia kiasi cha Shilingi Milioni 200 kwa ajili ya zawadi za fedha taslimu kwa  washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom huku bingwa akinyakua kitita cha Shilingi Milioni 70 ikilinganishwa na Sh 50 Milioni za msimu uliopita." Alisema Mwalim.
Mwalimu amesema lengo la kuongeza zawadi ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya wadhamini wa ligi na wadau wengine wa soka na kwa pamoja kuwa na dhamira ya dhati katika kuendeleza soka nchini.
"Kila mmoja ni shahidi wa namna ambavyo soka letu limekuwa na namana ambavyo tunakabaliana hatua kwa hatua na changamoto zinazohusiana na ligi. Ni matumaini yetu kwamba tunapiga hatua na tuna matumaini ya kufikia kiwango cha juu zaidi cha maendeleo ya soka nchini yanaonekana." Aliongeza Mwalim
"Kwetu sisi kama wadhamini tutajitahidi kadri inavyowezekana kuhakiksha tunaleta mabadiliko katika soka la Tanzania, tunaangalia mpira wa miguu nchini kwa upana zaidi kama mchezo unaopendwa, unaotuleta pamoja kama taifa na kuitangaza nchi yetu. Falsafa yetu hii imechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo utulivu na ushirikiano mzuri miongoni mwa wadau na hivyo kutuletea mafanikio." Alisema Mwalim
Zawadi nyingine zilizo tangazwa ni pamoja na zawadi ya mchezaji bora wa Mwaka golikipa bora, na mfugaji bora kila mmoja  anajinyakulia Shilingi Milioni 5.
Aidha, mwamumzi bora na kocha bora kila mmoja atajipatia Shilingi 7,500,000 kila huku timu iliyoongoza kwa nidhamu itapata zawadi ya fedha taslimu ya Shilingi Milioni 15.
"Tumekuwa na msimu mzuri uliojaa ushindani na hamasa, tunatarajia timu zitajipanga zaidi kwa ajili ya msimu ujao na hivyo kuendelea kuipa ubora ligi yetu."Alisema Mwalim huku akiwashukuru wadau wa mpira wa miguu nchini ikiwemo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi, Chama cha Waamuzi(FRAT), Vilabu, wachezaji na kipekee washabiki na kamati ya ligi kuu.
Amesema bila ya ushirikiano wa wadau hao na wengine ikiwemo Serikali, ligi kuu ya Vodacom isingeweza kufikia maendeleo iliyoyafikia katika msimu unaomalizika ambao kwa kiasi kikubwa ulitawaliwa na mpira wa uwanjani na si vinginevyo.
Viewing all 454 articles
Browse latest View live